Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,395
- 20,480
Marekani yapewa taarifa na Russia dakika 30 kabla, Ukraine na washirika wake washindwa kuizuia.
Ina uwezo wa kufika na kuangamiza mahali popote Ulaya nzima.
Hakuna mfumo wa kuizuia.
Ni Hypersonic hivyo inaweza kusafiri kwa kasi ya Mach 10 (kilometa 3 kwa sekunde, huwezi kuiona muenendo wake wa kasi kwa macho).
Inabeba vichwa vingi kwa mara moja ambavyo vikitawanyika huko angani kila kimoja kinaweza kujiongoza kufuata 'target' yake sehemu tofauti na vichwa vingine.
Russia imesema itakuwa inatoa taarifa kabla haijafanya shambulizi, tahadhari kwa raia eneo inalotaka kulishambulia waweze kuondoka lengo likiwa kupunguza maafa kwa raia wasiokuwa na hatia.
Muelekeo wa vita kati ya Ukraine na Russia umechukua sura mpya baada washirika wa Ukraine kuruhusu silaha za masafa marefu walizo wapa Ukraine zitumike kushambulia ndani ya ardhi ya Russia inayotambuliwa kimataifa.
Baada ya Ukraine kuzitumia hivi karibuni Russia amejibu mapigo kwa kuifanyia majaribio silaha yake mpya ya Oreshnik kwa kupiga kiwanda cha silaha cha Ukraine.
Ni teknolojia mpya ya Hypersonic Intermediate range ballistic missile.
Ina uwezo wa kubeba vichwa vya nyukilia (nuclear payload), kwa sasa imetumia vilipuzi vya kawaida(conventional bomb) lengo kutoa onyo tu. Pentagon wakiri silaha hiyo ni tishio lakini wana amini Ukraine itaweza kuhimili maafa yake.
Naomba wale wadau wa mambo ya silaha waje watoe maoni yao. Narudia, wale wadau wanaojua mambo ya silaha siyo shabiki wa vita vya Ukraine au NATO na Russia.
CC: T14 Armata waite wadau wengine tujadili wengine tujifunze.