Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 416
Raia wa Marekani aliyekuwa ametekwa nyara nchini Niger ameokolewa katika operesheni ya kijeshi iliyotekelezwa na Kkosi Maalum cha Jeshi la Marekani (US Special Force) karibu na mpaka wa Nigeria, vyombo vya usalama nchini Marekani vimethibitisha.
Raia huyo, Philipe Nathan Walton, alitekwa nyara na watu waliofika nyumbani kwake kwa kutumia pikipiki mapema siku ya Jumanne, huku wakidai fidia kutoka kwa baba yake aliyeishi kijiji cha jirani umbali wa kilometa moja kutoka katika eneo alipokuwa akiishi kijana wake.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema kuwa hakukuwa na mwanajeshi wa kikosi maalum aliyejeruhiwa katika operesheni hiyo, huku Rais wa Marekani, Donald Trump, akisema kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa jambo hilo lilikuwa 'ushindi mkubwa kwa wanajeshi wa kikosi maalum cha Marekani.'
Walton, ambaye anamiliki shamba karibu na mpaka wa Niger, hufuga ngamia na kulima maembe na anaishi na mkewe na binti yake mmoja. Shirika la Habari la Reuters liliripoti kuwa tkriban watekaji sita waliokuwa wamejihami kwa kutumia bunduki aina ya AK-47 walionekana kutoka katika jamii ya Fulani, lakini walizungumza Kihausa na Kiingereza, walimchukua Walton na kuwaacha mkewe na binti yake.
Afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutaka kufahamika amenukuliwa akisema kuwa tukio hili halihusiani moja kwa moja na ugaidi, bali ni utekaji uliofanyika kwa lengo la kupata fidia. Hakuna fidia yoyote iliyolipwa!
Tukio hili linakuja miezi miwili tu baada ya tukio lililohusisha kundi la kigaidi la ISIL kuwaua wafanyakazi sita wa kutoa misaada, raia wa Ufaransa na mwongozaji wao wa Niger wakati walipokuwa wakitembelea mbuga ya wanyama mashariki mwa mji wa Niamey.