Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 14,111
- 22,283
SIo siri hawa wanasiasa wanatuchezea, sisi maboss wao wanatufanya kuwa vijakazi wao, hatuna cha kuwafanya zaidi ya kuwaonyesha boss ni nani; Je Tutafanyaje ?
Box la Kura
Ndio huenda wataiba lakini wote / wengi tukiwakataa watajua ukweli kwamba tumewachokan na huenda wakajirekebisha, ila tutamchagua nani ? Ukizingatia hivi vyama navyo badala ya kutetea itikadi zao vimekuwa watetezi wa watu wao yaani imekuwa kama simba na yanga wao na sisi na kwa nguvu ya CCM ni vigumu kwa Chama kingine kupenyeza. Hivyo basi kama Kuchagua A au B hakuna tofauti kubwa tufanye nini.
Katiba
Kubadilisha Katiba mpya huenda kusifanyike leo wala kesho na mchakato ni mrefu, hivyo basi tungehakikisha kipengele kimoja tu kinabadilika. Mgombea Binafsi, hapo itatupa mwanya wa kuonyesha hasira zetu kwa waliopo na ambao wanafanya maamuzi yasio kwa manufaa ya Taifa bali manufaa ya genge lao, na tutawapa mwanya wale wenye mawazo mbadala kupata sehemu ya kukimbilia.
Operesheni Piga Chini
Hivyo basi kwa madudu yanayooendelea tutaweza kuonyesha hasira zetu kwenye Box la Kura, yaani hata kama muwakilishi ni mzuri kiasi gani ila kama yupo kwenye genge fulani na yeye apigwe chini. Kwanini unaweza kuuliza, (Sio tu kwamba Samaki mmoja akioza ila tunajua fika maamuzi yanayofanyika kwenye Genge mwisho wa siku ni kwa manufaa ya Genge)
Kura yetu kama Kadi Nyekundu
Kwahio mwisho wa siku Chama kitaelewa kwamba kwa madudu wanayofanya uchaguzi ujao tutakuwa na uwezo wa kukifutilia mbali..., na wale wazuri wote wanaweza wakajitoa huko kwenye Genge na Hata Rais pia aweze kuwa mgombea Binafsi akishinda atapick and choose kulingana na watendaji kutoka pande zote, na atakuwa sio part ya genge / magenge.
Huenda Uwezo wetu wa kuwapiga chini hawa walafi wasiovimbewa isilete maendeleo ila watajua kwamba come next election tunaweza kuwaondoa na kuchaguliwa kwao kwenye ticket ya genge lao haimaanishi ndio njia ya kwenda kujipatia kula
Huenda ninaota ila kuna Umuhimu wa kuwapiga Chini hawa walamba asali wote next election, hata kama sio kwa makosa yao bali ni kwa makosa by association, yaani ni kama kule gengeni kuna ugonjwa wa kuambukiza ambao inabidi kuuondoa wote wawekwe lock-down (away from politics / decisions).