Ongezeko la uvamizi wa magari binafsi kwenye barabara za Mwendo Kasi (BRT): Je, Mamlaka zinabariki matumizi haya?

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
765
939
Ongezeko la uvamizi wa magari binafsi kwenye barabara za Mwendo Kasi (BRT): Je, Mamlaka zinabariki matumizi haya?

Katika miaka ya hivi karibuni, mfumo wa Mabasi ya Mwendo Kasi (BRT) umekuwa suluhisho la kipekee la kupunguza msongamano wa magari mijini na kuboresha huduma za usafiri kwa wakazi wa maeneo ya jiji la Dar es salaam.

Hata hivyo, changamoto kubwa inayozidi kuongezeka ni uvamizi wa magari binafsi na vyombo vingine katika barabara za mwendo kasi zilizotengwa mahsusi kwa ajili ya mabasi hayo, hali hii haikubaliki na inaleta madhara makubwa kwa mfumo mzima wa usafiri, uchumi wa miji, na usalama wa abiria, pia kupelekea mabasi kuchelewa kufika katika vituo vya Mwendokasi kwa muda uliotarajiwa.

Uvamizi wa barabara za mwendo kasi unavuruga kwa kiasi kikubwa utendaji wa mfumo wa BRT. Mabasi yanapokutana na magari binafsi ndani ya njia zao, kasi ya mabasi inapungua, na hivyo kusababisha ucheleweshaji wa huduma.

Moja ya sababu kuu za kuanzishwa kwa mfumo huu ilikuwa ni kuhakikisha kuwa abiria wanaweza kufika wanakoenda kwa haraka zaidi na kwa uhakika. Uvamizi huu unafanya lengo hilo kutofikiwa, na matokeo yake ni hasira na malalamiko kutoka kwa abiria, jambo ambalo linaweza kupunguza imani yao kwa mfumo wa uendeshaji wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi.

Uvamizi wa magari binafsi kwenye barabara za mwendo kasi unaongeza hatari ya ajali. Barabara hizi zimeundwa maalum kwa ajili ya mabasi ya mwendo kasi, na zina viwango vya kiusalama vinavyotegemea aina ya magari yanayostahili kutumia barabara hizo.

Magari binafsi, pikipiki, na vyombo vingine vya usafiri vina muundo tofauti wa mwendokasi na uwezo wa kudhibiti mwendo, na hivyo vinaweza kuleta hatari ya ajali mbaya zinazosababisha majeruhi au vifo.

Hali ya uvamizi wa barabara za BRT inapelekea hasara kubwa kiuchumi. Mabasi ya mwendo kasi yanapolazimika kusimama au kupunguza kasi kwa sababu ya magari mengine, yanatumia muda mrefu barabarani, na hivyo kuongezeka gharama za uendeshaji kama vile matumizi ya mafuta.

Pia, abiria wanaochelewa kufika kazini au kwenye shughuli zao za kila siku wanapata hasara ya muda na rasilimali, jambo linaloathiri uzalishaji wa kiuchumi kwa ujumla.

Aidha, uvamizi huu unaleta dharau kubwa kwa juhudi za Serikali na mamlaka za usafiri za kuboresha miundombinu na huduma kwa wananchi. Serikali imewekeza mabilioni ya fedha katika kujenga barabara za mwendo kasi na kuanzisha mfumo wa BRT ili kuboresha usafiri wa umma.

Uvamizi wa magari binafsi kwenye barabara hizi ni ishara ya kuvunja sheria na kutoheshimu miundombinu iliyojengwa kwa ajili ya faida ya umma wote. Mamlaka zinazohusika kusimamia jambo hili ziko wapi au zimepatwa na Ganzi ipi kwa kukaa kimya ?

Ili kukabiliana na tatizo hili, mamlaka husika zinapaswa kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya wahusika wanaovamia barabara za BRT ikiwemo kutungwa kwa kanuni zinazotoa faini kali kwa wahusika ikiwezekana faini ya kuanzia Tsh 500,000/- na kuendelea ili kukomesha swala hilo maana mradi huu ukikamilika kwa phase zote unatakiwa kuleta tija na sio hali ilivyo hapa mwanzoni mwa utekelezaji.

Pia sheria zinazohusu matumizi ya barabara hizi zinapaswa kuimarishwa na kupewa uzito unaostahili. Faini kali na adhabu za papo hapo kwa wanaokiuka sheria ni njia moja ya kuhakikisha kuwa magari binafsi yanaheshimu mipaka iliyowekwa. Vilevile, matumizi ya teknolojia kama vile kamera za usalama na mifumo ya GPS yanaweza kusaidia kudhibiti hali hii kwa ufanisi zaidi.

Uvamizi wa barabara za mwendo kasi na magari binafsi si jambo dogo linalopaswa kupuuzwa. Ni tatizo ambalo linaathiri moja kwa moja ubora wa huduma za BRT, usalama kwa watumiaji, na uchumi wa nchi. Ni muhimu kwa jamii na serikali kushirikiana katika kulinda barabara hizi na kuhakikisha kuwa zinatumiwa ipasavyo kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

TUCHUKUE HATUA HARAKA!

IMG-20240905-WA0215(2).jpg
 
Maendeleo yanaanza kwa kuheshimu sheria. Magari binafsi barabara ya mwendokasi? Hii sio haki kwa wote!
 
Kwanza huo uchafu unaoitwa mwendokasi ni hasara Kwa serikali.Zimejengwa Kwa gharama kubwa Kwa Kodi za wananchi walizokamuliwa Hadi damu kuwa Toka lakini ufanisi wake ni sifuri.Kwa kuwa huu mradi umeonesha kushindwa kujiendesha ni Bora gari zote zipite kwenye hiyo miundombinu.Maana kupita kwao huko kwenye hizo miundombinu wanakuwa wamepunguza foleni kwenye hizi barabara tunazobanana.Mimi binafsi huwa nawasifu sana wanaopita humo.
 
Back
Top Bottom