matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,590
- 18,355
1: Matajiri ni matajiri sio kwa sababu wanafedha. Matajiri wanafedha kwa sababu ni matajiri.
Namaanisha nini? Wekeza kujenga uwezo wako pesa ni matokeo ya mindset za kitajiri. Na moja ya mindest ni kuamini kila pesa unayoipata hauipati ili uitumbue unaipata ili ilete pesa nyingine.
2: Boresha jinsi unavyoongea. Ongea kwa kumaanisha (speak with hyperintention). Katika viumbe na vitu alivyoumba mwenyezi Mungu ni wewe tu ndio ulipewa Lugha. Lugha yako inatusaidia tunaokusikiliza kujua wewe ni mtu siriasi, mwaminifu, ni wakupigwa, mpuuzaji, tapeli mtu makini au maneno mingi. Wekeza katika kuboresha namna unavyojieleza, itakusaidia sana kuaminika, kuuza, kupewa madili. Usiongee hovyohovyo.
3: Panga kula vizuri. Weka malengo ya kula vitu vya maana. Achana na soda, chocolates, sukari nyingi, mafuta mengi, Kula mbogamboga, mbegumbegu na matunda kwa wingi. Hii itakusaidia kujiamini kiafya. Hii itaathili akili, uwezo na itakupa nguvu ya kubaki katika uzalishaji bila kuchoka. Kimsingi huwezi kuwa na malengo makubwa wakati unakula ili ujiue mapema.
4: Punguza team yako. Scan ndugu, marafiki, jamaa, mates ambao wanakupa nguvu chanya, wanakutakia heri, wanakutia moyo kusonga mbele na hakikisha hawa ndio wanakuzunguka. Wanaokuonea wivu, wanaokuchukia, wanaokuvizia, wanaokushusha au wanaokutabiria mwisho mbaya hao waweke pembeni kabisa kwa upendo mwingi ila kwa kumaanisha. Hakikisha hawajui moves zako ili wakoswe cha kuhujumu.
5: Usisahau kusherehekea. Kila ushindi au hatua hata mdogo kiasi gani sherekea kidogo. Jitahidi sherehe zako unasherekea na familia yako. Baba mama na watoto kama wewe ni kama mimi ninayeamini katika baraka na uchanya wa familia. Mfano jana nilikuwa nasherekea hatua flani ndogo na vijana wangu na mama yao, tumetandika kanga wa kuchoma watatu na madikodiko mengine mbalimbali. Hii inaongeza nguvu chanya kwenye maisha.
6: Badili mfumo wa kununua vitu au kupata huduma kwa kuangalia gharama. Angalia thamani unayoipata kwenye huduma au bidhaa hiyo. Kuwa mtu wa thamani sio mtamaduni wa kuangalia wengine watakuchukuliaje ukionekana na kitu flani. Kama kinakuongezea thamani (value) katika mikakati yako nunuq
/chukuq/nenda/fanya kwa ujasiri wote na kwa kumaanisha, achana na watu watakuchukuliaje.
7: Ibada. Usiache ibada. Kimsingi chanzo cha utajiri ni muunganiko wa Juhudi binafsi na utegemezi wako kwa nguvu za Mungu. Hapa ndio utakuwa na maisha ya maana. Ukiwa na Juhudi bila Mungu utaishia kufanikiwa kiuchumi bila amani na utulivu. Ukiwa na Mungu bila juhudi utaishia kuwa masikini mwenye msongo wa mawazo t3na ambaye watu wanakukwepa.
Ni hayo tu.
Ongezea chochote na sisi tujifunze.