Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Wakili Onesmo Olengurumwa akizungumza na televisheni ya mtandao ya Sauti Digital.
"Sisi tulidhani na tulishauri sana kwamba serikali iwasikilize (CHADEMA), wawape ile fursa ya mazungumzo na bado tunaendelea kushauri kwamba CHADEMA wana hoja za msingi, wamepoteza ndugu zao, wamepoteza wenzao, na wengine mpaka sasa hivi hawajulikani waliko, ninadhani serikali iwasikilize, watoe nafasi ya meza ya mazungumzo ili kuepusha haya maandamano ambayo yamepangwa ambayo kimsingi maandamano hayo hata yakifanyika mwisho wa siku watarudi kwenye meza ya mazungumzo. Kwa hiyo msisubiri watu wafanye maandamano ndiyo mje mkae kwenye meza ya mazungumzo"
"Ushauri wetu ni kwa Mheshimiwa Rais, yeye mwenyewe kwa kutumia falsafa yake ya R-4 amekuwa akisisitiza kwamba serikali yake ni ya mazungumzo, kwa kupitia zile R-4. Kwa hiyo tunamshauri sana Mheshimiwa Rais, kwa kipindi hiki, kabla ya hiyo tarehe ya maandamano haijafika, kama kuna namna yoyote ile, atafute namna wakae na watu wa CHADEMA waone namna ya kuweka mikakati ya kutambua na kufahamu hawa ndugu zao waliopotea ambao mpaka sasa hivi hawajulikani wanapatikanaje. Ninadhani kwa kufanya hivyo kwa taifa ni afya zaidi lakini hata kwa kiongozi inakuwa inaashiria kuonesha uongozi bora zaidi"- Olengurumwa.