Ona maajabu ya Artificial Intelligence: Inamjua mpaka Maxence Melo

macho_mdiliko

Platinum Member
Mar 10, 2008
24,131
46,147
Hello members (wale ambao mlikuwa hamjui kama mimi)!

Niliposoma kuwa Elon Musk na wenzake wametafadhalisha kuwa Artificial Intelligence (kwa kifupi AI) isiendelezwe tena kwani ni hatari kwa binadamu sikutilia maanani sana mpaka nilipoanza kuitumia. Je, wewe umewahi kuchati nayo? Kama bado basi kuna hii inayoitwa ChartGPT! Ni free.

Unatakiwa tu uwe na email na ukishajisajili uko tayari kuuliza chochote. Inajua mpaka kiswahili. Inaijua mpaka Jamii Forums na zaidi inamjua mpaka Maxence Melo na mashtaka kukamatwa kwake.

Ona nimeuliza swali hili: ''Unamjua Maxence Melo wa jamii Forum?

Hili hapa ndiyo jibu iliyonipa ''Ndiyo, ninajua kuhusu Maxence Melo, ambaye ni mwanzilishi na mmiliki wa JamiiForums, jukwaa la mtandaoni la kijamii na habari lililopo nchini Tanzania. Maxence Melo amekuwa mstari wa mbele katika kukuza uhuru wa kujieleza na utetezi wa haki za kibinadamu nchini Tanzania, lakini pia amekuwa akikabiliana na changamoto za kisheria kutokana na shughuli za jukwaa lake. Mnamo mwaka 2016, Maxence Melo alikamatwa na kushtakiwa kwa mashtaka ya kuzuia upelelezi na kuchapisha taarifa za uwongo, lakini alifanikiwa kupata dhamana baada ya kuzuiliwa kwa muda mrefu.''
 
Hello members (wale ambao mlikuwa hamjui kama mimi)!
Niliposoma kuwa Elon Musk na wenzake wametafadhalisha kuwa Artificial Intelligence (kwa kifupi AI) isiendelezwe tena i za jukwaa lake. Mnamo mwaka 2016, Maxence Melo alikamatwa na kushtakiwa kwa mashtaka ya kuzuia upelelezi na kuchapisha taarifa za uwongo, lakini alifanikiwa kupata dhamana baada ya kuzuiliwa kwa muda mrefu.''
Naomba uniulizie unamjua macho_mdiliko halafu jibu niletee hapa kama ulivyofanya kwa max
 
Swali: Tundu lissu ni nani?
Jibu: Tundu Lissu ni mwanasheria, mwanasiasa, na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki nchini Tanzania. Alikuwa mwanasheria wa haki za binadamu na mwanaharakati kabla ya kuingia kwenye siasa. Aliwahi kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na amekuwa akijihusisha na masuala ya kupigania haki za binadamu, utawala wa sheria, na demokrasia nchini Tanzania. Lissu alijeruhiwa kwa risasi zaidi ya 30 mnamo Septemba 2017, na tangu wakati huo amekuwa akipata matibabu nje ya nchi. Hata hivyo, ameendelea kuwa mwanasiasa maarufu na msemaji mkali wa upinzani nchini Tanzania.
 
Swali: Yanga ni simba ni ipi timu nzuri
Jibu: Kama msaidizi wa AI, mimi sifanyi upendeleo kwa timu yoyote ya soka. Ni suala la mtazamo na upendeleo wa mashabiki wa soka kuhusu timu zipi ni nzuri zaidi. Yanga na Simba ni timu mbili kubwa za soka nchini Tanzania na zote zina mashabiki wengi na mafanikio makubwa katika historia yao. Kila timu ina uwezo wake na mashabiki wake, na inategemea mtazamo wa kila mmoja kusema ni timu gani nzuri
 
Swali: Umewahi kufika Tandale kwa Mpogole?
Jibu: mimi ni mfumo wa kompyuta na sina uwezo wa kufika mahali fulani kama binadamu. Hivyo basi, sijawahi kufika Tandale kwa Mpogole. Hata hivyo, niko tayari kushiriki taarifa ambazo ninazo kuhusu eneo hilo ikiwa unataka.
Swali: Haya eleza kuhusu Tandale kwa Mpogole
Jibu: Tandale kwa Mpogole ni eneo lililopo katika Kata ya Kijitonyama, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tanzania. Eneo hili ni maarufu kwa shughuli za biashara na makazi, na lina idadi kubwa ya watu wanaoishi katika eneo hilo. Tandale kwa Mpogole pia ni eneo la kihistoria kwa sababu lilikuwa sehemu ya mapambano ya uhuru wa Tanzania, ambapo viongozi wa Chama cha TANU walifanya mikutano na kufanya kampeni katika eneo hilo.

Kwa sasa, Tandale kwa Mpogole ni moja ya maeneo yanayokua kwa kasi jijini Dar es Salaam, na limekuwa likikabiliwa na changamoto za msongamano wa watu na magari, ukosefu wa miundombinu, na masuala mengine ya kijamii na kiuchumi. Hata hivyo, eneo hilo linaendelea kubuniwa na kuendelezwa ili kukidhi mahitaji ya wakazi wake na kuendelea kuwa sehemu muhimu ya jiji la Dar es Salaam
 
Swali: Unamjua Jemima Mrembo?
Imenijibu: Samahani, sina taarifa za kutosha kumhusu Jemima Mrembo. Je, unaweza kunitajia zaidi kuhusu yeye ili niweze kukusaidia kwa ufanisi zaidi?
Na kwakufanya hivyo tu! Ndipo anapozidi kupata taharifa zaidi! AI imepewa uwezo wa kujifunza yenyewe ni kama binadamu mtoto anakua akijifunza hili na lile, na kadiri tunavyo ilisha maswali nayo ndivyo inazidi kutafuta majibu na kuyahifadhi! Utofauti wake na binadamu wa kawaida ni kuota ndoto na nguvu ya kimaamuzi yani haiwezi kuwaza kama binadamu, bali ina pata reference kutoka kwenye data alizo meza
 
Uliza kama wanamfahamu Jemima Mrembo mtetezi wa wanawake wenye tabia nzuri kwenye ndoa zao
Mmeanza ku-tag mashost zenu, baada muda mfupi mnabadili muelekeo wa uzi kutoka kuwa mambo ya artificial intelligence na Kuwa kijiwe cha story zenu za mambo binafsi.
Utaona mtu anaanza kujiongelesha..
Nakuona shost ,habari za siku?.
Nipo, na mimi Nakuona!! Full bra brah.
Why msiende PM mjuliane hali ZENU?
 
Hello members (wale ambao mlikuwa hamjui kama mimi)!

Niliposoma kuwa Elon Musk na wenzake wametafadhalisha kuwa Artificial Intelligence (kwa kifupi AI) isiendelezwe tena kwani ni hatari kwa binadamu sikutilia maanani sana mpaka nilipoanza kuitumia. Je, wewe umewahi kuchati nayo? Kama bado basi kuna hii inayoitwa ChartGPT! Ni free.

Unatakiwa tu uwe na email na ukishajisajili uko tayari kuuliza chochote. Inajua mpaka kiswahili. Inaijua mpaka Jamii Forums na zaidi inamjua mpaka Maxence Melo na mashtaka kukamatwa kwake.

Ona nimeuliza swali hili: ''Unamjua Maxence Melo wa jamii Forum?

Hili hapa ndiyo jibu iliyonipa ''Ndiyo, ninajua kuhusu Maxence Melo, ambaye ni mwanzilishi na mmiliki wa JamiiForums, jukwaa la mtandaoni la kijamii na habari lililopo nchini Tanzania. Maxence Melo amekuwa mstari wa mbele katika kukuza uhuru wa kujieleza na utetezi wa haki za kibinadamu nchini Tanzania, lakini pia amekuwa akikabiliana na changamoto za kisheria kutokana na shughuli za jukwaa lake. Mnamo mwaka 2016, Maxence Melo alikamatwa na kushtakiwa kwa mashtaka ya kuzuia upelelezi na kuchapisha taarifa za uwongo, lakini alifanikiwa kupata dhamana baada ya kuzuiliwa kwa muda mrefu.''
Ni ipi Kati ya hizi??
Screenshot_20230330-164715.jpg
 
Back
Top Bottom