Pre GE2025 OMO: Zanzibar Hatutakubali Kura ya Siku Mbili 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
624
1,546
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Taifa, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema ACT Wazalendo haitakubali Zanzibar kufanyika kura ya siku mbili.

Mheshimiwa Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo leo Jumatatu Disemba 09 2024, aliposhiriki akiwa Mgeni Rasmi, wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Vijana wa ACT-Wazalendo wa Mkoa wa Kati Kichama, huko katika Ukumbi wa Chama hicho, Dunga Mkoa wa Kusini Unguja.

"Wajibu wetu ni kuilinda Katiba ya Zanzbar; kama ambavyo tuliahidi katika Kiapo, ili kupambania haki na kuwahudumia wananchi; hivyo tunaahidi 'Kura ya Mapema' haitojirudia Zanzibar".

Aidha, Mheshimiwa Othman amesema Chama cha ACT Wazalendo siyo Wakala wa Ajira kama wafanyavyo vyama vyengine, bali dhima yake kuu ni kupigania haki na maslahi ya watu wote, bila ya ubaguzi.

Amewahimiza Vijana kuacha kughilibiwa na kudanganywa, kwa kivuli cha kupewa ajira, na badala yake wasimame imara kutekeleza dhamira ya kuitafuta Zanzibar yenye Mamlaka Kamili.
IMG-20241209-WA0053.jpg
Wakitoa salamu zao, Katibu wa Taifa wa Vijana, na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Mkoa wa Kichama wa Kati, wa Chama hicho, Ndugu Muhamed Khamis Busara, na Ndugu Suleiman Ali Seif, kwa nyakati tofauti wamesema kuwa, 2025 ni Mwaka wa Maamuzi na wa mabadiliko, ambapo vijana kwao ni wajibu kuwepo mstari wa mbele katika kulifanikisha hilo.

Kongamano hilo ni mwendelezo wa Makongamano ya Ngome ya Vijana yanayoendelea, na yanayotarajiwa kufanyika Nchini kote, likibeba Kaulimbiu ya "Nafasi ya Vijana kuelekea Uchaguzi 2025 na Ukombozi wa Zanzibar".

Viongozi wa Ngazi mbali mbali wa Chama hicho, wamehudhuria Hafla hiyo, wakiongozwa na Katibu wa Habari na Uenezi Taifa, wa ACT-Wazalendo, Ndugu Salim Abdallah Bimani.
 
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Taifa, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema ACT Wazalendo haitakubali Zanzibar kufanyika kura ya siku mbili.

Mheshimiwa Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo leo Jumatatu Disemba 09 2024, aliposhiriki akiwa Mgeni Rasmi, wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Vijana wa ACT-Wazalendo wa Mkoa wa Kati Kichama, huko katika Ukumbi wa Chama hicho, Dunga Mkoa wa Kusini Unguja.

"wajibu wetu ni kuilinda Katiba ya Zanzbar; kama ambavyo tuliahidi katika Kiapo, ili kupambania haki na kuwahudumia wananchi; hivyo tunaahidi 'Kura ya Mapema' haitojirudia Zanzibar".

Aidha Mheshimiwa Othman amesema Chama cha ACT Wazalendo siyo Wakala wa Ajira kama wafanyavyo vyama vyengine, bali dhima yake kuu ni kupigania haki na maslahi ya watu wote, bila ya ubaguzi. Amewahimiza Vijana kuacha kughilibiwa na kudanganywa, kwa kivuli cha kupewa ajira, na badala yake wasimame imara kutekeleza dhamira ya kuitafuta Zanzibar yenye Mamlaka Kamili.
View attachment 3173189
Wakitoa salamu zao, Katibu wa Taifa wa Vijana, na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Mkoa wa Kichama wa Kati, wa Chama hicho, Ndugu Muhamed Khamis Busara, na Ndugu Suleiman Ali Seif, kwa nyakati tofauti wamesema kuwa, 2025 ni Mwaka wa Maamuzi na wa mabadiliko, ambapo vijana kwao ni wajibu kuwepo mstari wa mbele katika kulifanikisha hilo.

Kongamano hilo ni mwendelezo wa Makongamano ya Ngome ya Vijana yanayoendelea, na yanayotarajiwa kufanyika Nchini kote, likibeba Kaulimbiu ya "Nafasi ya Vijana kuelekea Uchaguzi 2025 na Ukombozi wa Zanzibar"

Viongozi wa Ngazi mbali mbali wa Chama hicho, wamehudhuria Hafla hiyo, wakiongozwa na Katibu wa Habari na Uenezi Taifa, wa ACT-Wazalendo, Ndugu Salim Abdallah Bimani.
chuki na uhasama baina ya vyama vya upinzani nchini itaendelea kua ndiyo chanzo cha ulegevu na hatimae kutokomea kabisa kwa nguvu na ushawishi wa upinzani nchini.

ACT wazalendo ni suala la muda tu itatokomea Zanzibar, na kwenye uchaguzi mkuu ujao haitakuepo tena kwenye srikali ya umoja wa kitaifa :pulpTRAVOLTA:
 
Back
Top Bottom