Ombi: Stendi ya Msamvu Morogoro iwekwe sehemu ya kupumzika abiria

Kapyarupyaru

Member
Nov 4, 2016
33
43
Hii stendi angalau inamuonekano mzuri kuliko ile inayojiita ya kimataifa pale Ubungo, shida kubwa katika kituo hiki cha Msamvu ni sehemu ya kumpumzikia abiria wakati wakisubiri usafiri, yaani abiria wanakaa chini kwenye ngazi au korido pamoja na kazi nzuri ilofanyika hili nalo lapaswa kuzingatiwa.

 
Hivi wajenzi walipitiwa ama?
 
Na magari yanayolazimika kulala pale abiria wake wanapata tabu kweli usiku, na pia pale kahama ni kero sana kwa magari yanayolala pale
 
Sasa stand Bila sehemu ya kupumzikia abiria inakuwa haijakamilika
 
yani hiyo stand iko poorly designed...architecht hajaumiza kichwa au hana exposure...ilikua ni suala la kugoogle tu angepata samples nyiingi kuliko hicho kituko....
 
Hilo lilitakiwa liwe kipaumbele cha kwanza kwenye michoro ya hiyo stand.
 
Kosa liko hapo na hili si kwa wakandarasi wa hapo tu bali karibia wote Tanzania
mwenye kosa hapo ni Architect/ msanifu majengo aliyedesign...kwa sababu mkandarasi yeye kazi yake ni kujenga kutokana na michoro ya mteja tu..though anayo nafasi ya kushauri of which anaweza akasikilizwa au asisikilizwe pia
 
Sasa humo ndani kwenye ghorofa na madirisha ya kioo kuna nini? Mabasi yamo humo au ?
 
mwenye kosa hapo ni Architect/ msanifu majengo aliyedesign...kwa sababu mkandarasi yeye kazi yake ni kujenga kutokana na michoro ya mteja tu..though anayo nafasi ya kushauri of which anaweza akasikilizwa au asisikilizwe pia
Poa asante kwa ufafanuzi
 
Mkichokonoa sana mtakuta mjengo wa kupumzikia abiria upo kwenye mchoro lakini pale stendi haupo na ukiuliza utapigwa sound kuwa madiwani waliridhia kupokea mradi ukiwa na mapungufu kwani pesa iliisha
 
Kuna siku niliambiwa hii ni phase one, bado two phases, let us hope kwenye hizo phase mbili zilizobaki kutakuwa na jengo la kupumzikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…