Kama kichwa cha habari kinavyojieleza
Hili ni ombi langu kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)
Pia nimeona vyema kuleta hapa JF ili kupata maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali
Katika matumizi ya simu inaweza ikatokea mmiliki wa simu akaipoteza simu yake bahati mbaya au simu hiyo ikaibiwa
Ombi langu kwa TCRA kwamba simu ambazo zitapotea labda kwa kudondoshwa, kuachwa sehemu au kuibiwa. Simu hizo zifungiwe matumizi yake ndani ya nchi
Mtu aliyepotelewa na simu akitoa taarifa ya upotevu wa simu atapewa taarifa ya upotevu ambayo ataipeleka TCRA pamoja na IMEI namba na namba ya simcard iliyokuwa inatumika katika simu hiyo baada ya TCRA kujiridhisha na kuthibitisha vielelezo vya umiliki wa simu hiyo nayo iweze kuifungia matumizi simu hiyo iliyopotea hapa nchini
Nakumbuka mwaka 2016 simu zote zilizokuwa feki zilizimwa na TCRA. Hapa inaonyesha mamlaka hiyo inaweza kufungia simu kwa sababu fulani
Jambo hili litasaidia kupunguza au kukomesha visa vya wizi wa simu na uhalifu wa kimtandao
**