Ombi kwa shirikisho la soka Tanzania (TFF)

vibertz

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
2,128
4,166
TFF tunaomba mfikirie umuhimu wa mashindano, ubora wa mashindano na vipaumbele vya mashindano. Kwasasa timu ya Simba na Yanga zina mechi muhimu sana ya klabu bingwa hatua ya robo fainali na inachezwa tarehe kati ya tarehe 29 na 30 mwezi huu. Lakini nimeshangazwa na kutaka kuwatumia wachezaji muhimu wa Simba na Yanga kwenye bonanza la FIFA series ambayo itachezwa tarehe 25 huko Azerbaijan.

Hivi kweli mmeshindwa kutafakari kuona umuhimu wa timu zetu za Tanzania kufanya vyema kwenye klabu bingwa kiasa kwamba hamkuona haya ya kuwaachia wachezaji wao waendelee na program za makocha wao kujiandaa na mechi ya klabu bingwa zilizopo mbele yao?

Yaani hili nalo ni mpaka mfundishwe? Au mnataka vilabu visiwe vinatoa ruhusa kwa wachezaji wao muhimu?

Kuna umuhimu wa viongozi wa Simba na Yanga kukaa chini na TFF kuomba kubakishiwa wachezaji wote waendelee na program za maandalizi ya mechi ya klabu bingwa na isitoshe katika wachezaji wataochukuliwa ni kutoka Tanzania pekee kwavile mataifa mengine yanatoka hawa wachezaji wa Simba na Yanga hayapo kwenye hili bonanza
 
Back
Top Bottom