Ombeni Sefue (OS), ombea haya yasikukute na wewe

MBATATA

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
542
209
Mtoto wa rafiki yangu ni Mwandishi wa habari wa chombo kimoja maarufu hapa Nchini. Baba yake ni kiongozi katika moja ya Taasisi kubwa za umma ambazo hivi sasa zipo katika kipindi kigumu cha kuchunguzwa na hatimaye kufanyiwa marekebishio al maarufu "kutumbuliwa majipu'.

Rafiki yangu ananiambia kila akipigiwa simu na mtoto wake huyo (Mwandishi) huishiwa nguvu maanake anahofu ya kuambiwa "Baba leo tulikuwa Ikulu kumsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi akitueleza maamuzi ya Rais"! Ingawa mtoto hajui, lakini baba mtu hubaki akikosa pumzi mpaka mtoto amalize salaam na kuaga ndipo apumue. Hili linanikumbusha hali ilivyokuwa Miaka ya huko nyuma.

Miaka ya 1990 nikiwa mwajiriwa wa serikali kama Karani katika wizara mojawapo yenye nguvu na kongwe, Serikali hii iliamua kuendesha
zoezi la kupunguza watumishi, maarufu kama 'Redundancy'. Viongozi wakuu walikuwa wakijifungia kwenye vikao vya siri kujadili mwenendo wenyewe na wakitoka huko Mkuu wa Utawala anakuwa amebeba kabrasha lenye maamuzi yote.

Siku zilizofutata Mwangalizi wa Ofisi (au OS yaani - Office Supervisor) alikuwa akiitwa kwa Mkuu wa Ytawala na kupewa kazi ya kusambaza barua kwa watu waliokuwemo katika orodha ya hao walengwa kwa kuwafuata maofisini na kuwakabidhi barua zao. Ama kweli kilikuwa kipindi kigumu, na huyo Bwana OS ilipokuwa akiingia ofisi fulani hali hubadilika kabisa na furaha na vicheko vinavyoendelea hutoweka kama chumvi kwenye maji.

Na huyo OS (ni Marehemu sasa - Mungu amlaze pema huko aliko - sijui?) alikuwa akisha ona utulivu na woga umeshawapata watu, husema kwa sauti ya mamlaka: "E,Ndugu fulani yupo hapa?" Mtume! Macho yote hukodolewa kuelekea kwa mwenzetu mtajwa masikini na kushuhudia anavyosainishwa barua huku akititetemeka kwa simanzi.

Acheni bana, siku hizo ajira serikalini ilikuwa na "security" ya nguvu, uhakika wa maisha. Basi huyo Bw. OS akiondoka huku nyuma huacha watu wakimfariji mwenzao huku wakijiuliza sijui kesho zamu ya nani tena?

Bwana OS aliifanya kazi hii kwa bidii, kwa kujituma na kwa kujiamini kwa vile aliona "mteule mahsusi' hadi akajenga tabia ya kuona ufahari fulani akiingia mahali na kuona watu wanapomwona tu wanatamani kujificha chini ya meza!

Siku ya siku naambiwa Bw.OS alienda kukabidhi Despatch Book kwa Mkuu, na kutoa taarifa kwamba amemaliza kazi ya kuwakabidhi barua walengwa wote. Baada ya kufanya hivyo Mkuu akamwambia "OS, umefanya kazi nzuri, sasa na wewe saini hapa uchukue barua yako!'

Bwana Sefue unavyoongea na waandishi huku ukichekelea kusema hayo uliyoagizwa (huwa nakuona ukitabasamu),angalia yasikukute kama haya ya OS huyo - labda kama unastaafu kazi kwa umri kesho kutwa!
 
Taarifa yako inasikitisha sana..Japo hata kama yeye atapewa barua ya kuachishwa kazi,utofauti ni mkubwa sana kati ya watendaji waandamizi wa serikali na watendaji wa ngazi za chini huku.Shock itakuwa tofauti na maisha yenye utofauti mkubwa yataanza kuonekans kwa watendaji wa chini kuliko hao wa juu kabisa.
 
Yeye hana makosa maana ndiyo kazi yake mkuu, hapo ni jukumu la watumishi wa umma kuacha tabia zao mbaya
Mkuu usiseme Hana makosa, yeye aliishatekeleza mengi ya JK. Tena anamakosa makubwa tu, kilichomuacha mkinga pale alipo ni ukila la kipofu usimshike mkono. Magufuli anamhitaji kwa ajili y kumpa umbea,bila bila umbea ikulu ngumu
Hatuniombei mabaya lkn muosha, huishwa.
 
Yeye hana makosa maana ndiyo kazi yake mkuu, hapo ni jukumu la watumishi wa umma kuacha tabia zao mbaya
Nadhani mleta mada hajalaumu Nazi yake Bali anazungumzia jinsi anavyoonekana katabasamu na kufurahia utumishi wa wengine unavyositishwa.
Anyway, labda anafurahi tuu ila kama sikosei Leo kuna kiongozi wa upinzani kamtaja yeye na vigogo wawili kama majipu makuu yaliyovia usaha. Tusubiri ushahidi utakapowekwa hadharani kama hilo tabasamu litaendelea.
Tukumbuke ktk hata yaliyotumbuliwa wapo ambao uchunguzi unaendelea na kama wako clean basi watarudi kazini
 
Watakaoumia na kuteseka ni watoto wao
viongozi dizaini za kusifiwa na kupendwa na ma Rais dizaini ya Magufuli hushindwa hata kuwa na biashara yeyote
hutegemea serikali asilimia 100...
watoto huja kuulizwa 'nyie si baba yenu alikuwa fulani'?
mbona mnaomba kusaidiwa tena?
waulize watoto wa Sokoine
 
yy ni mjumbe tu.....ulitaka akitumwa na mh presidaa agome kwa kuwa naye ataoshwa?
 
Baada ya kufanya hivyo Mkuu akamwambia "OS, umefanya kazi nzuri, sasa na wewe saini hapa uchukue barua yako!'
Bwana Sefue unavyoongea na waandishi huku ukichekelea kusema hayo uliyoagizwa (huwa nakuona ukitabasamu),angalia yasikukute kama haya ya OS huyo - labda kama unastaafu kazi kwa umri kesho kutwa!

Hapo (penye red) umeniacha hoi Mkuu! Ingawa sijui kama hilo laweza mkuta huyo OS, maana si unaona watu wanavyosema Mkulu anaendelea kuchota umbeya! Hata hivyo, kina Philemon Luhanjo waliishia vipi pamoja na kelele zoote zile!
 
Hata akitolewa si ana pensheni nzuri tu. Tatizo zamani watumishi walilemaa sana, walikuwa hawajiandai na kustaafu. Halafu hilo lidandasi la kipindi hicho lilikuwa na malipo kidogo sana.

Kuna ma kesi mengi sana yaliyotokana na lidandasi lile mengine bado hayajaisha mpaka leo, nafamu kuna mzee wangu wa kanisa alipigwa lidandansi mwaka 1994 huko TTCL, kesi bado inaunguruma to date
 
Kuna kaharufu ka ukweli hapa...ni sawa na kupewa dili la kuua kisha na wewe unauawa ili siri ibaki kwa mmoja tu aliyekutuma....muda utasema yote!
 
Hapo (penye red) umeniacha hoi Mkuu! Ingawa sijui kama hilo laweza mkuta huyo OS, maana si unaona watu wanavyosema Mkulu anaendelea kuchota umbeya! Hata hivyo, kina Philemon Luhanjo waliishia vipi pamoja na kelele zoote zile!
Huyo Luhanjo alipona kwa kuwa alikuwa anastaafu, na Ludovick Utoh - Mkaguzi Mkuu akawabeba wote. System ndio ilivyo lakini kwa Bw. OS tusubiri tuone.
 
Watakaoumia na kuteseka ni watoto wao
viongozi dizaini za kusifiwa na kupendwa na ma Rais dizaini ya Magufuli hushindwa hata kuwa na biashara yeyote
hutegemea serikali asilimia 100...
watoto huja kuulizwa 'nyie si baba yenu alikuwa fulani'?
mbona mnaomba kusaidiwa tena?
waulize watoto wa Sokoine
Wewe mbona hueleweki? Unamaanjsha nini hasa? Kwahiyo viongozi waendelee kula rushw na kupat visivyo halali yao?
 
Kweli kazi ni maisha bila kazi mtaa ni mgumu sana

Ila hatuhitaji hata lepe la huruma kwa viongozi wa awamu iliyopita wamechota sana bila huruma kwa nini sisi tuwahurumie?

Mpaka kugawana mabilioni kwenye sandarusi hata wakifukuzwa hawana cha kupoteza bado wana mikwanja ya kula bata mpaka na vitukuu vyao sina huruma nao kila napowaona watoto wa masikini kariakoo wanavyoteseka kuuza mfuko shilingi mia akale
 
Sefue ajistaafu anapewa shirika au ubalozi akale maisha , sefue ni mtu wa system huwa hawatupwi hawa jamaa.
 
Wewe mbona hueleweki? Unamaanjsha nini hasa? Kwahiyo viongozi waendelee kula rushw na kupat visivyo halali yao?


Siyo wote waliosimamishwa wamekula rushwa. Kuna kutoendana na kasi ya mh, kuna uzembe, kuna HISIA za rushwa na matumizi mabaya ya ofisi nk. Ni HISIA kwa sababu ni Mahakama pekee itamtia hatiani mtu kwa rushwa!
 
Back
Top Bottom