Olengurumwa: Licha ya jitihada zinazofanyika lakini zoezi la uokoaji Kariakoo lilikuwa 'slow'

Nyakijooga

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
263
468
Mratibu wa Mtandao wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu Tanzania, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kwamba licha ya jitihada ambazo zimefanyika katika zoezi la uokoaji kwenye gorofa liloporomoka Karikoo amedai kwamba zoezi hilo limeonekana kwenda taratibu (slow).

Akizungumzia tukio hilo November 18, 2024 Olengurumwa amesema kwamba inaonesha kwamba bado Taifa halijajiandaa kukabiliana na majanga kwa uharaka hasa kutokana na tukio hilo kutokea kwenye Jiji la Dar es Salaam, ambapo amesema kwenye eneo kama hilo jitihada za haraka zingepaswa kuonekana.

Soma Pia:
Aidha amesema kwamba kulingana na taarifa zilizopo inaonesha chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo ni ujenzi ambao ulikuwa unaendelea, ambapo amesema kuwa kulingana na taarifa hizo wanashauri mamlaka zinazotoa vibali kuwajibika ikiwemo kufanya ukaguzi wa miundombinu ambayo wanaitolea vibali mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom