chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Polisi vipi hawakuibuka?
Msemaji wa CCM christopher Ole Sendeka akiongea ofisi ndongo za CCM Lumumba Dar amesema kwenye mkutano mkuu utakaofanyika Julai 23 mwaka huu wanatarajia kuenzi mila ya chama cha mapinduzi kwa kumpa John Magufuli ambaye ni rais uenyekiti wa chama hicho siku hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa sasa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni rais mstaafu
weee. igp akitaka atumbuliwe fasta afanye huo mchezo.Vipi hapakuzingirwa na police?
Mmebadili gia sasa , hii mmebadilishia baharini si bureBasi mbadili katiba ieleweke mnazingatia mila na si katiba.
Kweli mkuu, hebu tusubiri tuoneIla mkumbuke huyo Dereva alikwishawahi kutamka wazi wazi mbele ya umma " Mimi siyo dereva, sijui kuendesha na wala gari sitaki kuliongoza na leseni sina" Leo hii mnataka kumkabidhi busi lililojaa abiria aendeshe kwa miaka 5/10. litafika salama kweli?
Busi=Bus=BasiIla mkumbuke huyo Dereva alikwishawahi kutamka wazi wazi mbele ya umma " Mimi siyo dereva, sijui kuendesha na wala gari sitaki kuliongoza na leseni sina" Leo hii mnataka kumkabidhi busi lililojaa abiria aendeshe kwa miaka 5/10. litafika salama kweli?
unadhani hajui alichoandika au? busi ni lahaja tu ambayo huenda ikatumiwa na jamii fulani, hata hivyo huenda ametumia lugha ya picha kuwasilisha mawazo yakeBusi=Bus=Basi
Ni kweli mkuu kama sisi wanachadema tunavyoteseka na Mila ya chama chetu, mbowe hana kabisa mpango wa kufuata kanuni ya chana, ... Siasa za Tanzania ni uozo tu hasa huku kwenye vyama ambavyo wanalilia demokrasia ya nchi wakati ya kwao ndani ya chama inawashinda..hivi kati ya mila ya chama na katiba ya chama kipi muhimu zaidi? huu uongozi wa kupeana utalitesa taifa letu...
Nilidhani mikutano imepigwa marufuku (hadi mahafali). Naona nilisahau kwamba CCM si chama cha siasa bali ni serikali. Nilisahau kwamba mkutano wa CCM ni sawa na mkutano wa baraza la mawaziri.
Msemaji wa CCM christopher Ole Sendeka akiongea ofisi ndongo za CCM Lumumba Dar amesema kwenye mkutano mkuu utakaofanyika Julai 23 mwaka huu wanatarajia kuenzi mila ya chama cha mapinduzi kwa kumpa John Magufuli ambaye ni rais uenyekiti wa chama hicho siku hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa sasa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni rais mstaafu
haa haa kwa kweli ni shida. chama kimekabidhiwa dola kuongoza bado kinavunja katiba yake. je kweli watalinda katiba ya nchi? kweli ccm iliondoka na nyerere mwenyewe.Ni kweli mkuu kama sisi wanachadema tunavyoteseka na Mila ya chama chetu, mbowe hana kabisa mpango wa kufuata kanuni ya chana, ... Siasa za Tanzania ni uozo tu hasa huku kwenye vyama ambavyo wanalilia demokrasia ya nchi wakati ya kwao ndani ya chama inawashinda..