Ole Sendeka: Lema tunajua wanaokulipa, soko la Tanzanite halitarudi Arusha kamwe

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,894
8,437
Mirerani. Mbunge wa Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amemtaka Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema kutokuhadaa wafanyabiasha wa madini ya tanzanite wa kutwa soko la madini hayo litarudishwa jijini Arusha, akisema kiongozi huyo anadandia treni kwa mbele.

Lema aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini na aliyerejea Machi Mosi akitokea nchini Canada alikokimbilia na familia yake mwaka 2020 akidaiwa kutishiwa usalama wake, amewaambia waandishi wa habari Machi 4 kuwa soko la Tanzanite halipaswi kuwa Mirerani pekee.

Ole Sendeka akizungumza kwenye ziara ya Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo mji mdogo wa Mirerani jana Jumatano Machi 8, amesema biashara ya madini ya tanzanite haitahama Mirerani kamwe.

"Lema asidandie treni kwa mbele kwa kuwaongopea wana Arusha kuwa soko la madini ya Tanzanite litahama Mirerani lirudi Arusha hilo halitafanyika.

"Kazi halali huwezi kuita ni laana kwani shughuli zozote za halali zinazomsababisha mtu kipato na kufanya mkono wa mtu uende kinywani huwezi kusema ni laana.

"Yeye amewadharau bodaboda mara viongozi wa dini, sasa anatapatapa kwenye tanzanite, ametoka huko Canada tunatambua anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo,"

Hata hivyo, Chongolo akikagua jengo la Tanzanite City Mirerani amesema.

"Hata hivyo, CCM siyo chama cha kujibizana na wanasiasa ila wanaoota mchana waacheni waote kwani serikali ya CCM haiwezi kujenga jengo kubwa la soko la madini Mirerani kisha lihamishe.

"Mirerani hivi sasa mpo kwenye jiji la tanzanite na jengo lilikamilika mtafurahia matunda ya rasilimali hii ambayo duniani inapatikana eneo hili pekee," amesema Chongolo.

Julai 7 mwaka 2021 Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akizungumza mji mdogo wa Mirerani aliagiza biashara ya Tanzanite ifamyike Mirerani pekee ili kuuinua kiuchumi mji huo na kudhibiti utoroshaji.
 
Back
Top Bottom