Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 216
- 993
Nimefika Ofisi ndogo za RITA Kindondoni mida ya saa 1:48 asubuhi kuchukua cheti cha Kuzaliwa cha Mtoto ukiwa umepita mwezi mzima tangu nitume maombi ya Mtandao na kuwa Approved.
Kinachoshangaza ni kuwa kwanza hakuna eneo la kutosha kukaa watu wanaosubiria vyeti hivyo. Mathalani, leo imenyesha mvua, kutokana na wingi wa watu ilibidi baadhi wanyeshewe mvua wakiwa wamesimama kusubiria huduma.
Wafanyakazi wa hapa hawajali muda wa kazi, vyeti vimeanza kutolewa saa 3. Jaribu kufikiria, umefika kufuata huduma siku ya kazi, wahudumu hawapo, umekaa kwa muda wa zaidi ya saa 1 unasubiria huduma huku unayeshewa na mvua. Hii haipo sawa.
Cha kusikitisha zaidi ni kuwa pamoja na status ya system kusema maombi yapo ‘Approved’ kwa muda mrefu, bado vyeti hivyo havipo tayari. Najaribu kuwaza, nini maana ya kumjulisha mtu kuwa maombi yake yapo ‘Approved’ anaweza kufuata cheti wakati cheti chenyewe hakijatengenezwa? Uhuni.
Bahati mbaya sana sikuwa peke yangu niliyeambiwa kusubiria maombi yarudishwe juu (nadhani chumba namba 39 kama sijakosea) yaende kuangaliwa upya. Baada ya kulalamika, mhudumu mmoja alifafanua kuwa watu tulioona wanapewa vyeti ni wale walioomba mwaka jana, na kwamba vyeti vya mwaka huu vilikuwa bado havijashughulikiwa.
Katika dunia ya sasa ya Mtandao, unacheleweshaje huduma muhimu kama ya cheti cha kuzaliwa kwa sababu zilezile za kipuuzi za siku zote za “Mtandao ulikuwa/upo chini?” Hii haikubaliki. Tukate vipi bima za watoto? Nimeamua kuondoka, nitarudi tena siku nyingine maana kazi zangu zinakwama.
RITA Kindondoni acheni uzembe. Hakuna sababu yoyote ya kueleweka mnayoweza kuitoa kama ‘Justification’ ya uhuni huu.