Mtoto Wabibi
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 451
- 294
Wacha waisome namba hawa Wahehe/Wagogo/Wamaasai/Wakulya/Wasukuma wa Jimbo la Isimani
Moja kati ya Majimbo Masikini sana niliyopata kutembelea..Mwaka 2013 nilikuwa nafanya utafiti kwa ajili ya masomo yangu,nilichagua eneo la Iringa na hususani Jimbo la Isimani.Niligundua mambo mengi sana,na hakika ni moja kati ya majimbo masikini sana katika Mkoa wa Iringa
Eneo la Isimani(Lwang'a,Nyang'oro,Mkungungu,Ngano na Usolanga) miaka ya 1980's lilifahamika kama "Basket of Tanzania",shuleni tukasomeshwa kilimo cha Mahindi Iringa-Isimani,limekuwa kame sana sana,watu wanalala na njaa na ardhi imekosa rutuba kabisa,uharibifu wa mazingira kwa kukata miti na kuchoma mkaa ni mkubwa sana,milima ya Nyang'oro iliyokuwa ina msitu mkubwa na vijito vinavyotiririsha maji imekatwa hovyohovyo.Kampeni za Shirika la "Concern" toka nchi za Scandinavia haijafua dafu kufufua upandaji wa miti na kutunza mazingira.Hakuna juhudi za Serikali wala nini kurudisha heshima ya Isimani ktk kilimo
Mbunge wao Lukuvi hakuna alichofanya,watu wanakunywa maji ya makorongoni na ngedere,huduma za afya hovyo,shule za hovyo,maji hakuna kabisa kabisa mfumo wa maji...Watu wanaenda kunywa maji ya bwawani zinapokunywa ng'ombe na punda.
Maendeleo mengi yameletwa na mashirika ya dini,Wamisionari wa kanisa katoliki ndio kama serikali huko Isimani,Ndio wanaojenga shule,kituo cha afya na huduma za maji.Aibu sana jimbo hili.Ukifika huwezi amini kama ndio Jimbo la William Lukuvi.
Bahati mbaya hata wasomi halina,hata hao wachache waliopo wamekimbilia Dsm na mikoa mingine ya Mbeya na kwingineko.CCM wasaidieni hawa watu wa Isimani,ni mafukara wa kufa mtu na wanawapa kula kila uchaguzi
Mkuu Mtoto Wabibi nimekaa hayo maeneo kama miezi miwili nikifanya utafiti,Study Areas ilikuwa Isimani na Ilula.Bila shaka wewe ni mwenyeji wa Isimani au mkazi kabisa yani umeeleza vizuri sana mazingira ya pale. yani huyu jamaa matatzo sana...! wasomi wapo wachache sana hata nao amewashika na vitisho vingi sana, akihisi tu unampinga utapata shida. Poleni sana wanaisimani jimbo masikini kuanzia watu( vichwani) hadi miundombinu...! chamndindi hadi ikengeza na mawindi maji hakuna barabara hakuna na msahau kabisa.Igula,mangawe ,uhominyi, holo, mangawe yani hali mbaya.hii kauli ya " NDI MGAYA SIIDA" imewaharibu sana.ISIMANI BADILIKENI lukuvi amewahadaa vya kutosha.yani upinzani hauna nguvu kabsa kwa jimbo hili. CHADEMA na ACT,vp huyu jamaa mnamuogopa?
Kweli Isimani ya Lukuvi.…Toka 1995-2020!!!isimani nimetamani kuitembelea sasa wacha nisake uhuru wa kipato nitakwenda isimani ya lukuvi
Yule jamaa wa Isimani Sekondari,walimuandika hadi kwennye gazeti la MAWIO...Anaitwa Mwalimu Aidan Kapinga,nasikia jamaa ana misimamo sana,alipokataa kutumika na chama dola wakati wa uchaguzi,LUKUVI akamtafutia zengwe la kumuhamisha na kumshusha cheo,kwa sasa kapelekwa shule moja huko ndani ndani Ifunda kama mwalimu wa kawaida,toka ukuu wa shule mpaka mwalimu wa kawaidakuna mkuu wa shule ya sekondari alihisiwa tu mpinzani..! duu kilichotokea saizi anajuta.JIPANGE SANA na ufanye uspy wko kmya kmya
Lakini mbona pale Iringa Mjini siasa za upinzani toka 1995 zipo active?Maana nakumbuka mwaka 1995 Iringa Mjini walimchagua Mfalamagoha Kibasa wa NCCR MAGEUZI....sasa Chadema imechukua halmashauri na Meya wao,ina maana hili halisambai mpaka huko Isimani?au ndio watu hata Tv hawana?Nabii hasifiwi nyumbani. Lukuvi ni moja Kati ya viongozi makini na wenye tija kwa taifa lakini hapaswi kuendelea kujifanya kulipigania taifa huku jimbo kwake kunadidimia.
Ndicho kilichomuangusha Mh Aggrey Mwanri jimboni kwake Siha. Alikuwa makin Sana kufanya maamuzi ya kinaibu waziri lakini jimboni kwake Siha akapasahau kidogo japo alijitahidi kwa nafasi yake. Uchaguzi ulipofika watu wakamporomosha na kumwachia Dr G. Mollel.
Bahati mbaya kama ulivyosema,huko Iringa wasomi ni wachache Sana vinginevyo Lukuvi angeshapigwa chini.
Yule jamaa wa Isimani Sekondari,walimuandika hadi kwennye gazeti la MAWIO...Anaitwa Mwalimu Aidan Kapinga,nasikia jamaa ana misimamo sana,alipokataa kutumika na chama dola wakati wa uchaguzi,LUKUVI akamtafutia zengwe la kumuhamisha na kumshusha cheo,kwa sasa kapelekwa shule moja huko ndani ndani Ifunda kama mwalimu wa kawaida,toka ukuu wa shule mpaka mwalimu wa kawaida
Hii inatokea katika nchi ambayo siasa inatumika badala ya weledi
Jamaa nasikia ana nyota ya Simba,akiongea tu mtu unatikisika,watoto waliandamana arudishwe lkn Lukuvi akatumia uwaziri wake kumuangamiza
Sema ndio vile jamaa nasikia upstairs yupo vizuri...alipangua hoja kama anateleza mlima Kitonga,wakaishia kumpoka cheo chake