KERO Ofisi ya TRA Mafinga ina huduma mbovu, wahudumu wana dharau wateja

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Black Butterfly

Senior Member
Aug 31, 2022
129
364
Nimefika kufanyiwa makadirio ya kodi katika Ofisi za TRA Tanzania Mafinga lakini tangu asubuhi wahudumu wanajizungusha tu mara huku mara kule, mara mtandao uko chini mara wahudumu wengine wako kuhudumia nje ya ofisi hivyo tuendelee kusubiri.

Hii hali ni kero sana nimeuliza wateja wengine hapa wanakalamikia utaratibu huo karibia kila wakija hapa wanakalishwa muda mrefu bila huduma.

Hebu mamlaka husika zifanyie kazi hili suala kwa haraka. Haiwezekani ofisi umeme ukikatika na Internet inakata eti UPS yao ni mbovu inasababisha Server zichelewe kusoma.

Mambo ya ajabu kabisa haya.
 
Jambo kingine mkuu wa TRA msiwaache wafanyakazi sehemu moja Kwa muda mrefu hii inaleta majungu kazini na Kwa wafanyabiashara, kuzoeana kunakuwa kwingi
 
Back
Top Bottom