Kuna wanaoamini Trump, Atakuwa Rais wa 45 wa Marekani Katika Uchaguzi wa Nov 2016, Iwapo Akishinda Tikiti kwa Chama chake huo utakuwa ndio ukomo wa safari yake ya Kujikweza, Ubaguzi na Kebehi
Hawezi Kushinda, Wanaomshabikia, Trump kwao Ni Kama Kioo, Anaakisi Tabia zao, Anasema maneno ambayo siku zote wangetamani Kusema Lakini Hawawezi. Trump Kumuita Ni Juha, Mbaguzi wa Rangi nk. Maneno ya Kwenye Kamusi hayana Uwezo wa Kusisitiza Ukweli huo. Siku za Usoni Naamini watu wenye Tabia Kama zake wanatakiwa waitwe kwa jina neno moja tu Trump!
On a much more serious Note, Trump hawezi Kushinda kwa sababu Zifuataza,
Marekani Kuna Vyama Vikuu Viwili, Na Vyote Viana Mambo Vimeegemea na Aina ya Wafuasi.
Republican:- Hawa Wanaegemea zaidi, kwenye (a) Uhuru wa Kumiliki Bunduki (a) Wanachukia Kodi (c) Kisirisiri ni Wabaguzi wa Rangi na Wanadharau sana Raia wengine wa Dunia. (d) Wengi ni wazungu, Wengi ni wa sehemu za Kusini, wengi hawajasoma, hata Kama wakiwa wamesoma ukiwasikiliza argument zao kwa Maswala mbalimbali Utatamani Kulia. (e) Wanadharau Sayansi (f) Wanapinga abortion (g) Wanashabikia sana Vita (h) Wanavaa Ukristo Begani. Theodore Roosevelt, Dwight David Eisenhower, Richard Nixon, George W Bush, George H Bush, Ronald Regan, Ni Baadhi ya Marais waliotokea Chama Hiki. Tangu Uhuru Chama Hiki Kimetoa Jumla ya Marais 18
Sasa Ukiwa Unataka Kugombea Kwa chama chao Ukiwa Mjinga sana Utajitahidi sana Kujihusisha na Maswala hayo hapo juu, ili Uwashinde wengine ambao nao wanataka chama Kiwape Tikiti. Ubaya Ni Kuwa Kuna Point of No Return au Mstari Ukiuvuka basi Utakasirisha Kundi ambalo Ni Muhimu sana Nitalitaja baadaye. Trump ameshavuka huo mstari 4X4
Democrats :- Hawa Wanaegemea zaidi kwenye (a) Kuheshimu Utawala wa sheria (b) Kuthibiti umiliki wa silaha (c) Kuruhusu mwanamke Kuamua juu ya Uzazi* (d) Wanajifanya Hawashabikii Vita(mara nyingi sio kweli) (e) Wanaamini Matajiri wanatakiwa walipe Kodi zaidi (f) Wangetamani Huduma za afya ziwe Bure (g) Wengi ni Rangi Mchanganyiko, Wengi wamesoma na Kama hawajasoma wanafikiri kwa Kichwa sio kwa maninii, Wengi wanakuwa ni wa sehemu za Kaskazini, Wengi ni wa Kipato cha Kati. (h) Bahati mbaya wanashabikia Ushoga. Franklin D. Roosevelt, Harry S. Truman, John F. Kennedy, Lindon Johnson, Jimmy Carter, Bill Clinton na Barack Obama Ni Baadhi ya Marais waliotokea chama Hiki. Tangu Uhuru Chama Hiki Kimetoa Marais 16
Pia Ukiwa Unataka Tikiti ya chama hiki lazima uonyeshe upo nao kwenye core-values zao. Pia Ukivuka Mstari Mwekundu Utawaudhi Lile Kundi Muhimu na Hutashinda.
Marais Wengine Jumla yao 10 Walitokea Vyama Vingine vya Wakati wa Uhuru ambavyo Vyote Vilishakufa zamani sana. (Nashangaa Ni lini CCM nayo Itakufa) Hili Nimechomekea Tu.
Kundi Lingine Ambalo pia Limeovalap Kidogo na Makundi hayo mawili hapo juu, Ni Kundi muhimu sana, La Watu au Wapigakura Independent ambao Mara Nyingine wanaitwa Swing Voters. Huwezi Kamwe Kushinda Urais Marekani Bila Kupata Kura za Kutosha Kutoka Kundi hili, Ili Ujazie na zile za Kundi lako la Msingi. Kundi Hili Linajumuisha. (2) WAROMANI KATOLIKI(2) WATU WANYE ASILI YA KILATINO(3) WAMAREKANI WEUSI(4) WASOMI NA WAKUFUNZI WA VYUO.
Sasa Wote Hawa Donald Trump Kawakorofoa, Anabeza weusi, Amesema Mbofu sana Juu ya Walatino, Ameingia Katika Mabishano na kumjibu Kunya Pope! Wasomi wanaona Kuwa Trump ni Juha, sasa Niambie Ni Muujiza wa Namna Gani Utamwezesha Kushinda? Ingekuwa Tanzania Ohhh yes Zingenyang'anywa Computer na Vijana Kadhaa Kuwekwa ndani, na maji ya Upupu, Kisha Mtu unatangazwa mshindi. Kwa Kuwa Marekani Mauzauza hayo hayapo. Safari ya Urais ya Trump Ni safari ya Mtu Aliyeshika Sinia La Dhahabu Akimpelekea Ushindi Hilary Clinton au Ben Sanders. Most Likely Hilary.