Nyongeza ya Mishahara kwa Watumishi wa Serikali kuanza Agosti 2023

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,136
1,956
Serikali imetangaza kuwa nyongeza ya mshahara ya kila mwaka itaanza kulipwa mwezi ujao.

Waziri katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Simbachawene aliyasema hayo jana, baada ya kuulizwa na Mwananchi kuhusu nyongeza ya mishahara iliyotakiwa kuanza kulipwa mwaka wa fedha Julai, mwaka huu.

Nyongeza hiyo ilitangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sherehe za wafanyakazi uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro, Mei Mosi mwaka huu.
Related

Ahadi hiyo ilikuja ikiwa ni miaka saba tangu kuondolewa kwa mfumo huo na Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli mwaka 2016.

“Wafanyakazi mambo ni moto… Mambo ni fire,” alisikika Rais Samia wakati akitangaza kurejeshwa nyongeza ya mishahara ya kila mwaka kwa wafanyakazi wa umma.

Samia pia aliwasihi wafanyabiashara kutoongeza bei za bidhaa, huku akiwaahidi wafanyakazi kuwa mambo mazuri yanakuja pasipo kutangaza hadharani nyongeza hiyo.

Jana, Waziri Simbachawe alisema kuchelewa kulipwa kwa nyongeza hiyo kunatokana kuchelewa kwa mchakato wa kubadilisha mifumo ya mishahara.

Alisema kutokana na mishahara kuanza kulipwa kuanzia tarehe 24, walichelewa kufanya hivyo Julai mwaka huu, hivyo wataanza kulipa mwezi ujao.

“Tutaanza kulipa Agosti mwaka huu na tutalipa pamoja na nyongeza ambayo haikulipwa mwezi huu,” alisema Simbachawene.

Kuchelewa kwa nyongeza hiyo, kumezua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa umma nchini juu ya utekelezaji wa ahadi hiyo.

Akilizungumzia hilo, Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Tumaini Nyamhokya alisema wafanyakazi walitarajia ahadi hiyo itaanza kutekelezwa Julai 2023, lakini haikutekelezwa.

Alisema Tucta lilichukua hatua za haraka kuwasiliana na waziri mwenye dhamana, George Simbachawene na kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Juma Mkomi ili kupata ufafanuzi wa jambo hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
Ngoja nijiandae kupandisha bei ya sukari, asali lazima wote tulambe.
 
Back
Top Bottom