Mimi ni die fan wa Young African, timu yenye soka safi East Africa 😃 na mabingwa wa makombe Tanzania Bara kama hautaki meza godoro, lakini pia napenda sana music na nina-sikio zuri sana kwenye kusikiliza nyimbo na kuzielewa pia.
Nowdays wasanii wengi wamekuwa wakiimbia hizi timu pendwa bongo wakiwa kama fans lakini pia sehemu ya kazi zao.
Sasa basi ukisikiliza hizi ngoma ni moja tu ambayo ya Yanga inaweza ku-run mbele ya ngoma 10 za Simba lakini zilizobakia hazitambi kabisa yaani. miaka ya nyuma kuna ngoma aliimba Pepe Kalee (Yanga Bingwa wa Mataifa), hii ngoma ni kali hadi kesho ukiipiga inasaund vizuri tu, alituheshimisha sana mabingwa wa nchi. Yule mzee aliimba vizuri na ali-dedicated kila kitu pale, kuanzia melody and vocal yake (kongole kwa Pepe Kalee).
Ila sasa wasanii wa kizazi hiki hawajatutendea haki sisi mashabiki wa Yanga kwenye tungo za Music (ngoma kali). Hii ni kuanzia kwa Konde boy (Harmonize), Nandy hadi Marioo na wengine pia bado hawajatoa ngoma ambayo utaweza ku-compete na za Simba na ikatoboa.
Hapa anagalau kidogo yule jamaa anaitwa Sir Jay aliimba (Ndio huyo huyo) hii ngoma inasound well atleast na unavibe nayo popote (apewe maua yake). Ila shida ni kwamba na yeye hana trending songs za kutosha ukiitoa hiyo, imekuwa tofauti na Tunda Man anavyoimbia Simba.
Ukisikiliza kwa makini ngoma anayoachia Tunda Man kuhusu timu yake ya Simba, jamaa anadedicate kila kitu ili ngoma ishibe. kuanzia melody na vocal na hata zile line za kutukera wapinzani na kusifia timu yake, jamaa amekuwa solid sana katika hili. Kila ngoma akiachia inakuwa noma.
Haya kuna lile goma aliimba Chibu (Simba kiboko yao), Hili song hata ufanyaje inakuimpress kuanzia soul hadi kichwa kinatikisika. Achana na hilo, sasa kuna hii ya sasa alioimba King Kiba (Mnyama), bwana hii ni trend song, kwa sasa imepoa kinoma kinoma. Kuna ile sehemu anaimba;
"We unamjua Simba Mnyama,
Wakimataifa Mnyama,
Wakimataifa Mnyama,
Huyo Utopolo Mnyama.."
Jamaa anaujua mziki kudadeki zake halafu kinachokera alikuwa ni shabiki wa Yanga huyu jamaa (nilisikia) sasa mbona hakutoa kama hili huku kwetu?
Sasa basi ninachojiuliza, hawa wasanii wanatuchukuliaje sie Yanga kwenye kuachia ngoma kali zaidi ya hizi? Tumechoka kusikiliza za nyimbo kali za Simba tu kila siku.
Nawasilisha.