Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,068
- 38,989
Jana Octoba 14, ilikuwa siku ya mapumziko Kwa shughuli za kiserikali huku nchi ikitimiza miaka 24 Tangu kifo cha Rais wa Kwanza wa Tanganyika na Tanzania na miongoni mwa waasisi wa Taifa hili.
Ni siku ambayo imetengwa maalum pia kuadhimisha kilele cha wiki ya Vijana nchini na kuhitimisha mbio za Mwenge kitaifa.
Kama Ilivyotegemewa, Jana ilikuwa siku ya kueleza sifa kedekede za Mwalimu Nyerere (Mwenye siku yake) kuhusu màtendo yake mema, maono yake, uthubutu wa kutenda na kuamua Kwa ajili ya watu wake, uunganishaji wa nchi kuwa Taifa la watu wasiobaguana, matumizi sahihi ya raslimali za nchi, bidii ya kazi, na kubwa zaidi viongozi kuishi viapo vyao Kwa ajili ya Nchi na Wananchi.
Jana tumeshuhudia "UNAFIKI" halisi wa viongozi wa nchi hii. Jana Kila aliyesimama alimwongelea Nyerere utadhani kweli ni mfuasi wake. Jana Nyerere alipambwa akapambika. Kiujumla maiti haongei lakini Mwalimu alipakwa mafuta Kwa mgongo wa chupa.
Ni Nani anayaishi maisha ya Nyerere Kati ya viongozi tulionao Sasa hata nusu yake tu? Ni Nani anayefuata falsafa na maono ya Hayati kiasi cha kukusanyika Tanga kuhubiri wasiyoamini?
Wote waliokuwa Tanga Wana ukwasi usioweza kufafanuliwa chanzo chake. Wamejaa unafiki wanapoingia na ni Wanafiki wanapotoka.
Kiujumla Wamekwenda Tanga wakiwa Wanafiki na wametoka Tanga wakiwa Wanafiki.