RAKI BIG
JF-Expert Member
- Apr 26, 2020
- 394
- 456
JOTO la mgombea urais ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limeendelea kupamba moto baada ya kuwepo tetesi kuwa kada wa chama hicho Lazaro Nyalandu anafikiria kujitosa kwenye kinyang’iro hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam (endelea).
Nyalandu ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati anakusudia kuungana na makada wengine kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu utajaofanyika Oktoba 2020.
Tayari Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na Dk. Maryrose Majinge wamekwisha weka wazi kuwa watatia nia ya kuwania nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema, utiaji nia ulianza tarehe 3 hadi 15 Juni 2020.
MwanaHalisi Online limedokezwa na watu wa karibu wa Nyalandu kwamba atajitosa kuwania nafasi hiyo.
“Nyalandu anajitokeza kugombea, sijajua ni lini atatangaza nia lakini anajipanga kabla ya tarehe 15 Juni 2020 atatangaza nia,” kimedokeza chanzo hicho
Nyalandu aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini kuanzia mwaka 2000 alitangaza kung’oka ndani ya chama hicho tarehe 30 Oktoba 2017 na kujiunga na Chadema.
Nyalandu alizaliwa tarehe 18 Agosti, 1970 mkoani Singida ambaye katika kipindi cha miaka takribani ya 15 ya ubunge kuanzia mwaka 2000 hadi 2017 alishika nafasi mbalimbali akiwemo waziri wa maliasili na utalii.
Alipata elimu ya msingi katika shule za Pohama na Mrumba zilizoko kijijini kwao Singida na kuhitimu mwaka 1987.
Aliendelea na masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Kibaha mkoani Pwani (1988 –1991) na alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma kidato cha tano na sita.
Wakati akiwa mwanafunzi wa sekondari, Nyalandu alikuwa kiongozi wa juu wa Ushirika wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania(Ukwata) 1991–1993 na baadaye alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania walioteuliwa kuzuru jiji la Rio De Janeiro, Brazil na kushuhudia mkutano wa Mazingira mwaka 1993.
Nyalandu alipata elimu yake ya Chuo Kikuu nchini Marekani ambako alihitimu Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Usimamizi wa Biashara (BBA) mwaka 1997 katika Chuo Kikuu cha Wartburg.
Kabla ya hapo alikuwa amepata Shahada ya Biashara ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Wardorf nchini humo.
Mwanasiasa huyo, ana Shahada ya Uzamili aliyoipata kwa njia ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Buckingham, Uingereza akifuzu katika masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diplomasia.
Baada ya kuhitimu masomo yake ughaibuni,Nyalandu alianza kazi huko huko Marekani katika Benki ya North West, akifanya kazi katika kitengo cha operesheni za kibenki kati ya mwaka 1998–1999.
Aliporejea nchini Tanzania alifanikiwa kuwa sehemu ya washauri wa mke wa aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa, katika uendeshaji wa taasisi ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
Ushauri wa timu yake ulisaidia taasisi hiyo kupata misaada mingi kutoka nchi za Ulaya, Marekani, China na nyinginezo.
Pia, alikuwa anamsaidia mama huyo katika uandishi wa hotuba zake pale alipokuwa na majukumu makubwa ya kitaifa na kimataifa.
Nyalandu amemwoa mrembo wa Tanzania mwaka 2004 ‘Miss Tanzania’, Faraja Kotta na wana watoto wawili, Sarah na Christopher.
Alikuwa mstari wa mbele katika kusaidia Jamii katika masuala ya Elimu na Afya, ambapo alikuwa Mwanzilishi Mwenza wa Shirika la STEMM ambalo limesomesha wanafunzi zaidi ya 10,000 kwa kuwalipia ada za Sekondari, na baadhi yao kuwapa ufadhili katika Vyuo Vikuu.
Aidha, alisaidia kuwapeleka Nje ya nchi kwa matibabu watoto walionusurika katika ajali ya busi la Lucky Vicent iliyotokea Mei 2017 na kusababisha vifo vya wanafunzi na walimu zaidi ya 30.