Bashir Yakub
Member
- May 27, 2013
- 96
- 1,744
NUSURA YA CHADEMA ILIKUWA NI LISSU KUSHINDA TU.
Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.
Isingekuwa rahisi kwa watu wa Lissu kuungana na Mbowe kama Mbowe angeshinda lakini ni rahisi kwa watu wa Mbowe kumuunga mkono Lissu, na huenda wameshamuunga mkono hadi sasa.
Lissu, Heche,Lema na watu wao walikuwa wamefika mwisho pale Chadema na walikuwa na chaguo moja kati ya mawili, washinde wabaki au washindwe waondoke. Zile kauli kutoka kambi ya Mbowe kuwa "HAKUNA KUHAMA CHAMA" hakika ziliwalenga wao.
Kama hawa wangeondoka hakuna shaka CHADEMA ingefuata njia ya NCCR na CUF.
Mbowe kisiasa alishakufa mda mrefu alisubiri tu kuhitimishwa na sanduku la kura.
Fikiria kutoka kuwa na washauri kama wakina Prof. Baregu, Prof. Mwandosya,Dr.Azavel Lwaitama, Jeneral Ulimwengu hadi kuwa na mshauri mkuu kama JASUSI la kimataifa from Mbutu Republic Kigamboni, na Boni yai. Kuna interval kubwa hapa.
Wakati mwingine viongozi hujikuta wameingia katika udikteta bila kujua kwasababu mbili.
Moja, kuzipenda sana taasisi zao na kuamini kuwa akiondoka yeye taasisi itakufa, na Pili ni hii kauli ya " Wananiomba Niendelee".
Ukiona wewe ni kiongozi popote kwenye taasisi ama dola na yanaanza kukujia mawazo kuwa ukiondoka huenda taasisi ikaharibiwa, ama kuwa huoni anayefit kukurithi, basi haraka tema mate chini na sema "SHETANI PITA MBALI".
Raha ya shetani huwa ni kuona mwanadamu akifedheheka na wote waliofikiri hivi mwishoni walifedheheka. Shetani wengine ni hawa wanaokwambia kuwa "Bado tunakuhitaji endelea". Hawa ukishafedheheka huwa wanahamia upande wa pili.
Mbowe hajastaafu, ameshindwa uchaguzi. Chumvi tuite chumvi kadhakika sukari. Tuite vitu kwa majina yake.
Wanaomwambia Mbowe kuwa AMESTAAFU ajue tu wameamua kumpa heshima ila hajastaafu AMESHINDWA uchaguzi. Huu ndio msamiati sahihi waulizeni vizuri Bakita.
Mtu kitabu chake chote kacopy na kupaste maandishi ya watu, na kitabu tangu kinazinduliwa mpaka sasa kipo kwenye OFFER atakuwaje mshauri wako mkuu na akuvushe, haiwezekani.
Aki ya nani hawa vijana sijui walifaulu vipi kumlaghai mwenyekiti mzee wa watu.