1. Magufuli aliomba akafie nyumbani kwake, maana alisema hawezi kupona.
2. Alishangaa nilipomwambia sina mamlaka ya kuruhusu hilo.
3. Aliomba aitiwe Paroko wake, Pd Makubi na Kard. Pengo ambao walifika na kumpa upako wa wagonjwa!
4. Alikata roho mbele yetu wakuu wote watatu wa vyombo vya usalama.
5. Makamu wa rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi hawakuwepo Dar. Tukaamua kuwaita Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi ambao walifika na kuwapa taarifa ya msiba.
6. Ilibidi tutumie njia nyingine kumjulisha makamu wa rais ambaye ndiye alitakiwa kutangaza taarifa ya msiba.
7. Kulikuwa na mjadala kipi kianze kati ya mazishi na kumwapisha makamu wa rais kuwa rais.
8. Wengi walishauri yafanyike mazishi kwanza, lakini nilishauri uapisho uanze kwanza, kwa sababu marais wa nchi nyingine walitakiwa wapokelewe na rais wa nchi.
9. Lilikuja suala la gwaride la uapisho ambapo walishauri kusiwe na gwaride. NILIWAKATALIWA kwa sababu aliyekuwa anaapishwa ni amiri jeshi mkuu,na lazima bendera ya amiri jeshi mkuu ipandishwe kwa gwaride. Kinyume na hilo, jeshi LISINGEMTAMBUA kama amiri jeshi mkuu.
10. Kulikuwa na baadhi ya mawazo, kwamba inakuwaje juu ya makamu wa rais kushika nafasi ya urais. Nadhani walisahau kuwa katiba ya nchi inasema nini, ikiwa rais aliye madarakani anafariki au akishindwa kuongoza. Nami nilisema ni vema utaratibu huo ukafuatwa na ni jambo jema.