NSSF kipi ni kipi sasa kuhusu hili Fao lenu la Uzazi?

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
576
876
Niliona wanatangaza kuwa Mwanamke ukiwa umechangia miezi 36 na miezi 12 ya mwishoni ukiwa umechangia mfululizo unastahili hili fao la uzazi, na pia kuna sehemu nyingine nimeona wanasema hata baada ya kujifungua unaweza kuomba ndani ya siku 84 baada ya kujifungua.

Cha kushangaza mimi natimiza miezi 36 ya uchangiaji mwezi huu na natarajia kujifungua mwezi 3 mwanzo ni,wiki iliyopita nimeenda kufuatilia Maafisa wake wananiambia sina vigezo nilistahili kutimiza miezi 36 nikiwa na miezi 6 ya ujauzito au nyuma ya hapo na nilitakiwa kuomba wakati huo,na yote haya niliambiwa yakiambatana na huduma mbaya sana inayozuia kuhoji zaidi.

Ninachojiuliza mbona wanachotangaza na kinachotendeka ni vitu viwili tofauti ukweli ni upi? Kwanini haya yasiwekwe kwenye Matangazo yenu?

WanaJF mwenye uelewa au ushauri zaidi juu ya hili naomba msaada wenu nimekwama.

Halafu NSSF mbona hamna huruma na wajawazito kabisa?Nimeona wamejaa kwenye foleni wamechoka mnawakalisha hadi jioni na huduma zenu na lugha zenu mbaya na bado hawafanikiwi na hakuna anayejali,kwanini msiweke msimamizi wa ubora wa huduma eneo lile kutokana na unyeti wake?
 
Walishafilisika siku nyingi wanaishi kwa kudra za allah wanatoa wapi hela za kuwapeni wazazi, yaani raha upate wewe then wao wakupe mafao, thubutuuuuuuu mamifuko ya hifadhi ya jamii yako hoi sana ni ubishi tu unawaweka mjini jiwe alishakomba jkila kitu kule akasepa na kijiji chake
 
Niliona wanatangaza kuwa Mwanamke ukiwa umechangia miezi 36 na miezi 12 ya mwishoni ukiwa umechangia mfululizo unastahili hili fao la uzazi, na pia kuna sehemu nyingine nimeona wanasema hata baada ya kujifungua unaweza kuomba ndani ya siku 84 baada ya kujifungua.
Nenda ukomuone meneja wao, achana na hao wengine. Maana ukiuliza watu 3 kati yao nao watakupa majibu matatu tofauti.
 
Back
Top Bottom