ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 59,564
- 70,214
Hapa anajifanya anatoa ushauri na blaa blaa kibao ila yote hii ni nongwa maana Hawa ndio walitamani Kila kitu kiporomoke Ili wapate pa kumnangia mwanamke mwenzao ππππ
Unajaribu kujiuliza hayo aliyoekeza Profesa wa Rio De Janeiro ya Bukoba yataikumba Tanzania tuu ila huko kwingine ambako Sarafu zao ziko imara zaidi ya Dola hayatokei? Unagundua tatizo ni nongwa.
Sasa wameanza kutoka mapangoni na ramli kibao, wengine wanadai Trump akiapisha Dola itabadilishwa Kwa Shilingi 3,000 na ndogo zingine nyingi tuu kisa wivu.
----
THAMANI YA DOLA NA UHABA WAKE KUGEUKA GHAFLA NA IKAWA NI SHILINGI YA TANZANIA INAYOPANDA THAMANI. KULIKONI?
Tatizo la kuyumbayumba kwa sarafu katika mfumo wa soko huria ni jambo lisiloepukika lakini si kwa kasi kubwa inayoendelea. Benki Kuu ina jukumu na mbinu za kuingilia kuthibiti hali hii kuepusha athari zake kiuchumi , kibiashara na kulinda ajira.
Benki Kuu hukabiliana na tatizo kwa kuongeza upatikanaji wa sarafu inayopungua katika mabenki ya biashara ili kutunza uimara na utulivu wa sarafu yetu.
Katika nchi inayoendelea kama Tanzania na inategemea biashara ya nje (exports) athari za thamani ya sarafu yake kupanda na kuwa na nguvu dhidi ya dola ni kupunguza ushindani wetu kuuza bidhaa nje kwani wanunuzi wataona ni aghari na kwenda kununua kwingineko.
Mazao yetu ya kuuza nje yaweza kukosa masoko na bei za wakulima kushuka na pia watalii kupungua. Viwanda vyetu vyaweza kushindwa kushindana na bidhaa zitakazoingizwa kwa wingi kutoka nje hivo kuua uzalishaji wetu na ajira.
Ukuaji wa uchumi utapungua kutokana na ukosefu wa mzunguko mzuri wa fedha. Mahala pa kuanzia ni kwa Benki kuu kupunguza riba ili kuongeza fedha katika mzunguko kwenye benki za biashara. Riba za tarakimu mbili hazijakaa sawa. Zinaathiri uchumi. Tumezizoea lakini si sawa.
Chanzo: Tibaijuka na shilingi kuimarika
My Take
Ukweli ni kwamba Uchumi wa Tanzania ya Samia umeimarika sana na Kwa taarifa Yao utazidi kuimarika mwakani na Dola kushuka zaidi.
Hakuna Dua la kuku kumpata mwewe,wataumbuka zaidi ππ
View: https://x.com/BankOfTanzania/status/1867472805081887169?t=CyfW35iDASPhJ8pX_EaVWw&s=19