ACT Wazalendo: Abdul Nondo amekutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,828
13,585
WhatsApp Image 2024-12-04 at 16.13.20_9d943c25.jpg
Abdul Nondo akutwa na kiwango kikubwa cha sumu mwilini

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT-Wazalendo Taifa Ndg. Abdul Nondo jana tarehe 03 Disemba 2024, alifanyiwa upasuaji mdogo kwenye unyayo baada ya madakatri wanaomuuguza katika hospitali ya Aga Khan kubaini uwepo wa mivunjiko midogomodogo iliyotokana na kuumizwa vibaya wakati alipotekwa na baadae kutelekezwa katika ufukwe wa Bahari wa Coco Beach jijini Dar eSalaam.

Aidha Madaktari wamedai mwili wa Abdul Nondo unaonyesha kuwa na kiwango kikubwa cha Sumu ambayo mpaka sasa hawajajua kama zimetokana na athari za kupigwa na kuteswa au kama alipewa kitu chenye sumu na watekaji wake.

Kutokana na hali hiyo Uongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, umewaomba madaktari kumfanyia Uchunguzi zaidi kwa ajili ya kubaini aina ya Sumu iliyo mwilini mwake na kama zimetokana na kupewa Sumu
Kwa sasa hali ya Mwenyekiti Abdul Nondo bado si nzuri, mikono yake imevimba na ana maumivu makali mwilini japo madaktari wanaendelea kupambana kuhakikisha afya yake inaimarika na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Tunawashukuru watanzania wote kwa maombi yenu kwa Mwenyekiti wetu, tunaomba tuendelee kumwombea wakati madaktari nao wakiendelea kupambana kurejesha afya yake katika hali ya kawaida.
 
Back
Top Bottom