No offence: Siku nyingine tuwasaidie watanzania kwa njia hii!

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,394
4,748
Nimefarijika na moyo wa kujitolea kwa wote walio jitoa kuwasaidia majeruhi wa ajali kutoka shule ya lucky vincent.

Kamwe sitabeza juhudi za wote waliojitoa na kujitolea lakini funzo na maoni yangu ni lazima liwafikie wote wenye nia njema.

Tumesikia kuwa majeruhi wa ajali hiyo walionusurika kwa bahati ya pekee wanatarajiwa kupelekwa marekani kwa matibabu zaidi.

Hakuna aliyejiuliza ni sababu zipi hasa za kuwapeleka watoto hawa marekani.

speculation za wengi wetu ni kuwa imeshindikana kuwatibu hapa hapa nchini.

lakini kwangu mimi kama mtaalamu wa afya naamini uwezi na vifaa vya kuwatibu watoto hao upo hapa hapa nchini...katika hospitali zetu hizi hizi na kwa upekee sana hospitali ya MOI au KCMC .

Kuwapeleka nje ya nchi ni matakwa ya kisiasa au kijamii tu.

Anyways sitaki kulaumu lakini nataka kutoa somo tu.

Next time wasamaria hawa waliojitolea naamini kwa moyo wa dhati kabisa ni vizuri wakajiongeza kwa kutambua diagnosis ya mgonjwa na ultmate management yake.

hili litawasaidia sana katika kufanya masmuzi ambayo yatakumbukwa sio na jamii ya kawaida tu bali hata jamii ya wataalamu.

Ambacho hawajakifanya na pengine wangeweza kukifanya kwa manufaa ya watoto hawa na wengine watakaotokea pamoja na kuweka legacy ni hiki ninachotaka kukisema...

Wasamaria hawa wangefanya fundrising kama wanayojaribu kuifanya ili kuleta vifaa tiba husika na pengine wataalamu kutoka marekani ili kuwatibu majeruhi hawa hapa hapa katika hospitali ya mt meru.

Hili kingejenga uwezi kwa wataalamu wetu kwa ajili ya future events zinazofanania na hili.

Pia tungeweza kuiwezesha hospitali ya mt meru kuweza kupambana na aina ya wagonjwa mithili ya watoto hawa.

Hili ndio ninaloliita legacy kutokana na tukio hili.

Huu ni ushauri wangu mchungu kwa wasamaria wema ambao nadhani bado wako kwenye position ya kurectify...

cc: Nyalandu

RIP little angels...Get well soon three little angels
 
Wabongo bwana,
Yani umepewa lift unataka kupiga na Honi.

na kwa tabia zenu za kula rambi rambi mnatamani hata huo msaada wa kutibiwa hao vijana ungeletwa kwa cash.
by the way unafananisha vipi matibabu ya mount meru na ya marekani ?
kuanzia vifaa, watu na mazingira hivyo vitu ni Giza na mwanga.

wacheni tamaa!
iko siku kwenye .... mtakaaa kaimba Madee!
 
mkuu una uhakika kwamba jamaa hawajafanya utafiti kuwachunguza juu ya majeraha hayo yalowapata watoto? kwamba wameamua tuu kuwapeleka watibiwe marekani,afu pia hali za hao wagonjwa unafahamu ziko vp?
au labda pengine wameamua kuwapeleka huko ili kama kuna huduma bora zaidi watoto hao watibiwe haraka na warudi kuendelea na masomo,kwa sababu ajali hiyo ilikuwa kubwa na ya kitaifa so inawezekana wamepewa priority kwa namna ya jambbo au hali ilivyokuwa?
 
Unapewa lift karibia kufika!!
una uhakika gani hapo kwenye huo mchakato watu hawali?

Matibabu ya magonjwa ni universal ...yaani ukivunjika mguu dawa yake ni kuunganisha tu na kama imeshindikana kabisa kabisa basi utakatwa....MOI wapo madaktari wenye uwezo huo pengine wenye uzoefu mkubwa sana wa kupokea wateja wenye hali mbaya kuliko huko USA...

Kwa jicho la mwanajamii na mwanasiasa ni rahisi matapeli kuwarubuni.
 
Nasema uamuzi wa kuwapeleka huko ni wa kisiasa na kijamii zaidi...I dont see any proffesional Dr who would advice and refer to USA instead of MOI or KCMC or Agha Khan Nairobi.
 
Kwenye emergency assistance huwezi weka long term plan. Hayo ni ya baadaye.
Emergency assistance is to avoid unnecessary movement of unstable patient as much as possible.Kwenye emergence situation ndio sehemu sahihi kabisa ya kuamulia long term management...naongelea kiutabibu zaidi.
 
Usikurupuke, elewa content
 
Well said
 
Mnatibu paralysis secondary to spine injury? Kama hamtibu basi wenzetu kwa kutumia stem cell s wameanza majaribio ya kutibu paralysis inayo sababishwa na kuumia spine...matibabu ya spine injury hayapo advanved hapa bongo....na kwa nature ya ile ajali very likely wale watoto walipata sine injuries pamoja na injuries nyingine
 
Unaposema kisiasa una maanisha nn? Unajua nan kawatafutia wake watto nafas ya kwenda kutibiwa marekan?unajua nan aliekodi ile ndege kutoka marekan? Unajua nan anagharamia matibabu yao? Kama hujui nyamaza na kama unajua unachokiona tofauti ni kipi? Unadhan kila kitu ni siasa tu,kwa hyo hata kama wanaweza kutibiwa hapa na vifaa tunavyo je kuna ubaya gan kwenda kutibjwa sehem yenye uhakika zaid ya hapa? Pamoja na kwamba madaktari mpo hapa lakin mmeacha lin tabia za kuwadharau na kutowasikiliza wagonjwa kwa wakati? Mtu anakuja mahututi hamumtib mpka tupate karatas ya polis nawe dr umekaa tu unachat kwa jf,,waache wakatibiwe,waache wazaz wao wakaone dar la trump wakipona haraka hamtaacha kuja na maneno mengine tofaut na haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…