NMB App mna shida gani Leo?

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,743
7,078
Hivi hii benki kuwa hivi hapa nchini yenye kutengeneza mabilioni ya faida kila mwaka ni ya kumiliki app yenye kusumbua wateja kwa siku nzima wakisaka huduma?

Hivi kitengo chao Cha IT kinawawajibika ipasavyo?

Imagine, nimelipia huduma kwa nmb app na pesa wamekata ila hazijafika nilikozielekeza! Nimejitumia pesa kwenye simu, wamekata lakini hazijenda tigopesa ili nizitoe kwa matumizi na hawajatoa taarifa yoyote ya kuwepo kwa tatizo hili ili tutafute alternative nyingine.

NMB semeni lolote au rekebisheni matatizo ya mfumo kabla ya saa nne usiku huu vinginevyo nitawashitaki kwa kuilaza familia yangu na njaa na kunidhalilisha kwa washikaji kugongea nauli ilihali nimecommand service na mmeibana! Nitawahama baada ya kudai fidia.
 
Kwa waliopata the same changamoto tujuane hapa tuungane kuishitaki nmb kwa kutuzuia kupata huduma kwa wakati.

Nilishamtag mwanasheria wangu na amenihakikishia kuwa Hilo ni kosa kuwa kisheria kwani wameyaathiri maisha yangu binafsi na wategemezi wangu hivyo Kuna uwezekano wa kulipwa fidia kuwa tu.

Hivi ningekuwa nimezihamisha fedha kulipia huduma za matibabu, mgonjwa si atakufa kwa kunyimwa matibabu? Hebu wawe serious na fedha zetu!
 
Malalamiko yako yanaweza hata yasihusiane na app, pengine labda ni kutokana na uelewa mdogo wa mifumo...

NMB App >> Mfumo wa kibenki wa NMB >> Mfumo wa mtandao mwingine wa fedha (tiGOPesa, Mpesa etc)...

NMB App is just an interface, kama umefanikiwa kufanya hatua zote pasipo app kukwama wala kukuletea error message maana yake app haina shida...

Pesa yako inaweza ikawa imetoka kwenye mfumo wa NMB, lakini ikashindwa kureflect kwenye mfumo wa kifedha wa mtandao wako...

Imagine, nimelipia huduma kwa nmb app na pesa wamekata ila hazijafika nilikozielekeza! Nimejitumia pesa kwenye simu, wamekata lakini hazijenda tigopesa ili nizitoe kwa matumizi na hawajatoa taarifa yoyote ya kuwepo kwa tatizo hili ili tutafute alternative nyingine.

Na ukisoma maelezo yako hapa, inaonesha tatizo lipo kwa mfumo wa pili, huko pesa ilipopaswa ipokelewe...
 
Malalamiko yako yanaweza hata yasihusiane na app, pengine labda ni kutokana na uelewa mdogo wa mifumo...

App is just an interface, kama umefanikiwa kufanya hatua zote pasipo app kukwama wala kukuletea error message maana yake app haina shida...
Sidhani kama ni uelewa wa mfumo. It happens sometimes. Unafanya transaction App hailete msg kesho yake unatumiwa Msg transaction declined. Ni usumbufu
 
Mkuu naona unatoa shutuma kwa kupata changamoto peke ako.

Mimi nusu saa iliyopita nimenunua luku kupitia app yao.
Jion kama saa 12 hivi nimegonga miamala.

Usikute destination ndo shida. Lakini pamoja na hayo tupo dunia ya 3 hizi benk zinategema network providers, ama partneship za kibiashara kama hivyo tigo, voda n.k

Tuwe wavumilivu ama kuwa na mbadala kutatua changamoto zetu. Tusibakie kulalama tu wakati tunaweza kuwa na utatuzi wenyewe.

Hizi kampuni zinahitaji sana hela zetu ili zipate faida, hivyo usitarajie zikaacha hizo changamoto.

Mfano tu kutokuwa hewani unajua ni pesa ngapi zinatopotea kwao kama income?

Hawa tigo, voda ni mara ngapi wanakuwa hawapo hewani, unadhani wanapenda kuendelea kukusanya hela zetu.

Nilichojifunza ni kuwa mvumilivu inapobidi, lakini kutokutgemea huduma ya aina moja kuipata sehemu moja tu.

Pole sana.
 
Sidhani kama ni uelewa wa mfumo. It happens sometimes. Unafanya transaction App hailete msg kesho yake unatumiwa Msg transaction declined. Ni usumbufu

Kupokea SMS bado ni mfumo, sababu anayekutumia SMS sio NMB bali mtandao wako wa simu, NMB hana Telecom infra...

Wewe kama mteja wa NMB unachopaswa kuhakiki ni je pesa imekatwa kwa kutazama "taarifa fupi kwenye app yako ya NMB"...
 
Back
Top Bottom