Rose Mayemba
JF-Expert Member
- May 7, 2012
- 721
- 1,017
Ni katika mkutano wa mwisho wa kufungia kampeni za kumsaka diwani wa kata ya Njombe mjini katika jimbo la Njombe Kusini ambalo kwa sasa linaongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama ANNA MAKINDA.
Mh Silinde ambaye ni mbunge wa jimbo la Mbozi Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia ndiye aliyepewa dhamana ya kuhakikishwa ushindi unapatikana kata katika kata hiyo aliongoza maandamano makubwa yaliyokuwa na msisimko na mwamko mkubwa sana.
Maandamano hayo yaliyofanyika huku mvua kubwa ikinyesha yalihudhuriwa na wakazi maelfu kwa maelfu wa kata ya njombe mjini.
Hii ilipelekea chama cha mapinduzi kushindwa kabisa kufanya mkutano wao hivyo kukimbilia polisi kuomba msaada ili kusitisha zoezi la msafara wa CHADEMA.\
Haikufua dafu kwani viongozi walijipanga vizuri na waliwashinda polisi kwa hoja na kuendelea na msafara wao huku polisi wakighairi na kuanza kulinda msafara huo.
Hivi ndivyo ilivyokuwa leo katika picha
Polisi walipovamia msafara wa CHADEMA
Wananchi wa kata ya njombe mjini wakishangilia bila kujali mvua iliyokuwa inatiririka bila kikomo.