Njombe: Ashikiliwa na polisi kwa kumuua mtoto wa miaka saba akidhani ni ng'ombe

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
747
2,115
Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia Mwanamke mmoja aitwaye Estaroda Kaduma (28) amkazi wa Kichiwa kwa tuhuma za kumuua Mtoto wa Kaka yake anayefahamika kwa jina la Brown James Kaduma (7) ambaye anasoma darasa la kwanza katika Shule ya msingi Kichiwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema Kijana huyo alikuwa amelala majira ya saa nane usiku wakati Shangazi yake akiwa anafanya maombi lakini cha kushangaza alianza kupambana kwa kumpiga Mtoto akidhani ni ng’ombe mkubwa mweusi aliyefika wakati akifanya maombi.

“Huyu Dada huwa ana tabia ya kufanya maombi na katika maombi yake akaona ng’ombe mkubwa mweusi amefika katika eneo ambalo anafanya maombi, akaacha maombi akaanza kumpiga huyo ng’ombe na baadaye akatoweka baada ya muda akaonekana amefariki Kijana mdogo Mtoto wa Kaka yake baada ya kukanyagwakanyagwa kichwani na kujeruhiwa sehemu nyingine za mwili”

Kamanda Issah amesema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina na kutoa wito kwa Wananchi kuachana na imani hizo ambazo zimekuwa zikileta madhara makubwa kwenye jamii.
 
Mungu amlaze mahali pema lakini na ndugu zetu muwe makini kiasi, sio unaomba usiku wa manane ukisikia hata ndege analia nje unaongeza maombi kwa kudhani ni wachawi 🤦🏽‍♂️🤦🏽‍♂️
 
Back
Top Bottom