SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,768
25,084
๐“๐š๐ง๐ณ๐š๐ง๐ข๐š ๐ง๐š ๐ฆ๐š๐ ๐š๐ข๐๐ข ๐ฒ๐š ๐€๐ง๐ฌ๐š๐ซ ๐š๐ฅ-๐ฌ๐ฎ๐ง๐ง๐š.

- ๐๐ฃ๐ข๐š ๐ฒ๐š ๐Š๐ข๐›๐ข๐ญ๐ข ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐๐š ๐ค๐ฐ๐ž๐ง๐ฒ๐ž ๐ฅ๐š๐š๐ง๐š ๐ฒ๐š ๐‚๐š๐›๐จ ๐ƒ๐ž๐ฅ๐ ๐š๐๐จ.

- ๐–๐š๐ญ๐ฎ ๐ฐ๐š๐ง๐š๐จ๐ค๐จ๐ญ๐š ๐ฆ๐ข๐ข๐ฅ๐ข ๐ง๐š ๐ฏ๐ข๐œ๐ก๐ฐ๐š ๐ฏ๐ฒ๐š๐ค๐ž ๐ฉ๐ž๐ฆ๐›๐ž๐ง๐ข.

๐’๐„๐‡๐„๐Œ๐” ๐˜๐€ ๐Ÿฌ๐Ÿญ:

Tarehe 20 mwezi huu wa tano, waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Dkt. Stergomena Tax analiambia bunge kuwa hali ya usalama katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji bado haitabiriki.

1b1abd33bed7316106496c08d28e385f.png


Kwa maneno machache bado hali si shwari na sababu ni uwepo wa kikundi cha kigaidi cha Ansar Al-Sunna ambacho kinafanya mashambulizi huko nchini Msumbiji, jimbo la Cabo Delgado linalopakana na mipaka ya kusini mwa Tanzania.

Hivyo ni bayana, kama kikundi hiki bado kinahema, basi hatuna uhakika wa usalama wetu huko mpakani. Waulize wakazi wa vijiji vya mpakani, Kitaya na Michenjele, huko halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara juu ya USIKU ule.

Usiku huo wa tarehe 14/10/2020, giza halikuja mpweke kwenye ardhi yao bali liliambatana na wageni wasiowatarajia.

Ikiwa ni majira ya saa moja, wanatahamaki wamo katikati ya mashambulizi ya kundi kubwa la watu wenye silaha za moto.

0ec4a424da4ae2d14e3edae96c7d87fa.png


Watu wanakimbia huku na kule wakipiga mayowe ya hofu. Wavamizi wanachoma nyumba, magari, zahanati na pia ofisi ya kata.

Sekeseke la zaidi ya nusu saa. Kifo ama uhai.

Hali kuja kutulia, watu wanatoka walikojificha na walikokimbilia, wanakuja kuokota miili ya wenzao waliopigwa risasi na wengine waliochinjwa kama kuku.

Lakini mbaya, wanabaini wapendwa wengine hawapo. Wamebebwa wakaongozana na 'mabwana' wale kurudi huko walikotokea. Wengi wao wakiwa mabinti wa makadirio ya miaka 14 mpaka 20.

(pichani ni mwanaume aliyepoteza mke na mtoto wake wa kwanza)

c4dcc907b466a5499dd5f499f6430da7(1).png



Baada ya wiki moja kupita, siku ya Alhamis tarehe 22 Oktoba, ndo' aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Simon Nyakoro Sirro anasimama mbele ya vyombo vya habari na kusema tukio lile lilifanywa na magaidi waliovuka mpaka kutoka nchini Msumbiji.

957e775224010f55f3cc41b3d043edf3.png


Magaidi hao walikuwa 300 kwa idadi na wamefanya uhalifu ikiwemo mauaji. Baadhi wakakimbia na wengine wakakamatwa wanaendelea na mahojiano. Anasema lengo ni kupata mtandao wote wa magaidi.

Mtandao ulioanzia kule MKIRU (Mkuranga, Kibiti & Rufiji).

Kwa mujibu wa kamanda Sirro, wale Ansar al-sunna waliopo Msumbiji leo hii jimbo la Cabo Delgado, ambao ndo' wanamfanya waziri Stergomena Tax kusema kuwa usalama hautabiriki mpakani mwetu na Msumbiji, mtandao wao ulianzia hapa nchini mkoa wa Pwani.

Ila ni kweli Pwani tu? Kuna mahusiano gani na kwanini tena jimbo la Cabo Delgado mpaka leo hii? Mbinu za hawa magaidi ni zipi? Jeshi la SADC na Rwanda wamefikia wapi? Hali ya sasa ipoje na Rwanda ananufaikaje na mgogoro huu?

Ikumbukwe ripoti ya hivi karibuni, tarehe 17 Aprili 2024, kutoka gazeti la serikali ya Msumbiji, 'Boletim da Republica' imetolewa orodha ya watu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kushirikiana na kikundi hiki cha ugaidi, miongoni mwao wametajwa watanzania wawili; bwana Ally Yusuf Liwangwa (47) kutoka Dar es Salaam na bi. Safina Maulana (36) kutoka Mtwara.

7da9ce5539074fdaaab118d36e41aff2.png


Sasa turudi kwenye siku ile ya tarehe 5, Oktoba 2017. Siku ya kwanza kabisa risasi kurushwa hewani kwa jina la Ansar al-sunna.

Siku hiyo katika mji wa pwani - Mocimboa de Praia - jimbo la Cabo Delgado, mambo yanabadilika ghafla katikati ya usiku na alfajiri.

b8ed672a7b2bb9cfdf80f969b2766fae.png


Kuanzia saa saba ya usiku, kundi la watu wanaokadiriwa thelathini kwa idadi wakiwa na silaha za moto na baridi, wanavamia mji huu wakilenga vituo vya wanausalama.

Mpaka kufikia saa kumi alfajiri, vituo vitatu ambavyo ni Mocimboa district police, kituo kidogo eneo la Awasse na kituo cha polisi cha maliasili na mazingira vinaripoti kushambuliwa na kutokea majibizano ya risasi.

220px-Mocimboa_da_Praia_June_2020.png

ad8a8890c8ea25811810ebeb00e446ae.png


Msemaji wa jeshi la Polisi, kamanda Inacio Dina (pichani), anawaambia waandishi wa habari mashambulizi hayo yamepelekea vifo vya maafisa polisi wawili na wavamizi watatu lakini ripoti zinasema watu 14 walifariki na pia vituo viliripoti kupotelewa na silaha.

dinafile-1.png


Wavamizi hao walikuwa wanazungumza lugha ya Kireno, Kiswahili na Kimwani. Hiki Kimwani ni lugha ya watu wa pwani ya eneo hili.

Kamanda anasema pia wamefanikiwa kuwakamata wavamizi kadhaa na hao watasaidia kupata taarifa zaidi ya wavamizi wenzao.

Kamanda anapoulizwa kuhusu mafungamano ya wavamizi hao na waislamu wenye itikadi kali mathalani Al-shabab wa kule Somalia, anasema ni mapema sana kusema hivyo. Watu hao kutumia 'local languages' za hapa Msumbiji kunamaanisha ni watu waliokulia hapahapa.

photo_2020-03-27_08-54-12.png


Na hili linatukumbusha miezi sita nyuma ambapo redio ya taifa, Radio Mozambique, iliripoti kukamatwa kwa wanaume watatu wanotuhumiwa kuwa na 'connection' na Al-shabab.

Wanaume hao walikuwa wanawakataza watu kwenda vituo vya afya vya serikali na pia kuwapeleka watoto wao shule.

GNmjeTdW0AInBcg.png


Lakini baadae walikuja kuthibitika hawana mahusiano yoyote na Al-shabab ya Somalia japo wakaazi walikuwa wanawaita jina hilo, hivyo wakaishia kushikiliwa kwasababu ya kusababisha mashaka ya usalama.

Kamanda Inacio anawaondoa hofu wananchi akisema kikosi maalum cha kupambana na ugaidi kipo kazini na hivyo hali ya usalama itakomaa hivi punde.

Lakini tofauti kabisa na anachosema, huu ndo' unakuwa mwanzo rasmi wa mfululizo wa mashambulizi na mauaji katika jimbo la Cabo Delgado mpaka kuja kuvuka mpaka wa Tanzania.

a1359f7b0437c610128f7ca600d00d04.png


Kabla ya mwezi Oktoba kuisha, 'mabwana' wanamjibu kamanda kwa mashambulizi mawili katika kijiji cha Maluku na karibu na kijiji cha Columbe.

Mwezi unaofuata (Novemba) tarehe 29 wanavamia vijiji vya Mitumbate na Maculo. Wanaharibu kanisa na pia wanachinja watu wawili.

895d79603d940489d3ec93c5fa97afc5.png


Tarehe 13 January 2018 wanaingia mji wa Palma na kumwaga risasi sokoni na kwenye ofisi ya serikali. Watu watano wanakufa.

Tarehe 12 March, wanavamia kijiji cha Chitolo na kuchoma nyumba hamsini pia wanaua wakazi. Na kwa siku tatu mfululizo 20, 21 na 22 mwezi Aprili wanavamia vijiji kadha wa kadha wakiua na kuteka watu.

37a72a6672f64d5274bb1d5ed2d65b36.png


Ni mwezi unaofuata, Umoja wa Afrika (AU) unathibitisha ripoti ya gazeti la Afrika Kusini iliyosema kuna wapambanaji wa Islamic State wamekwishaingia ndani ya Msumbiji, ripoti ambayo serikali ya Msumbiji ilikuwa inapingana nayo hapo awali.
images(15).jpg

Na kilichofuatia baada ya hapo, ndo' hali ikawa mbaya zaidi. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huo 2019, watu zaidi ya arobaini na sita wakaripotiwa kuuawa kwa risasi na kuchinjwa kama kuku ikiwemo watoto wadogo.

6afd4fa6b6358326bae73df0dffa76f6.png


Achilia mbali nyumba lukuki ziliishia kuchomwa moto, watu kujeruhiwa na wengine kutekwa.

Si polisi, si jeshi la Msumbiji (FDS) wote wako hoi.

Mabwana hawa waliwavua nguo, kila mtu akaona uchi wao. Namna walivyo duni kwenye vifaa na mafunzo, na namna walivyo 'corrupt'.

61c7385fccbba22ce4f7daa5403206bd.png


Wananchi wanasema mara kadhaa wameshuhudia wanajeshi wakikimbia eneo lao la ulinzi muda mfupi kabla ya eneo hilo kushambuliwa na magaidi. Wengine wanaiba mitumbwi ya wananchi ili wakimbie kujinusuru.

Kwa kaliba hii, mashambulizi yanazidi kutiririka, magaidi wakiamua wachinje ama wakatekate kama kuni (dismembering).

Zoezi hilo linaenda mpaka mwishoni mwa mwaka 2019 ambako serikali ya Msumbiji inakiri kuhitaji msaada, wamezidiwa.

Kwa kupitia FDS wanawekeana mkataba na jeshi la mamluki (mercenary) Wagner Group la nchini Urusi, na kwa mara ya kwanza kabisa mapema ya mwezi Oktoba mwaka 2019, mashambulizi ya kwanza ya FDS wakishirikiana na Wagner Group yanashika hatamu na yanaleta mafanikio.

d9e0731ad8289d43ca738b8ccbfb1c36.png

Wanawakimbizia magaidi huko misituni na wanafanikiwa kukamata watu makumi kwa makumi walokuwa wanasafiri kutoka jimbo la Nampula kwenda kuongeza nguvu ya magaidi huko jimbo la Cabo Delgado.

Lakini nguvu hii ya soda haikuchukua hata mwezi. Magaidi wanajibu kwa mtindo wa mashambulizi ya kushtukiza (ambushing) na FDS wanapoteza wanajeshi ishirini huku Wagner wakipoteza wanajeshi saba.

Mwezi wa kumi na moja, FDS wanapoteza tena wanajeshi kadhaa huku Wagner wakipoteza wanajeshi watano.

75647a61fb4a0d8d43f595fdc70eadfa.png


Kipigo hiki kinapelekea pande hizi mbili, FDS na Wagner Group, kuingia kwenye mgogoro. FDS wanailaumu Wagner kutokuwaheshimu maafisa wao na huku Wagner wanalaumu jeshi la FDS pamoja na raia kuwa 'undiscplined'.

Hivyo oparesheni inafeli.

Wagner wanaondoka zao na katika ombwe hili, mkuu wa jeshi la Polisi, kamanda Bernadino Rafael, anaona afanye jambo upesi ili kujiimarisha kiusalama.

Anawasiliana na bwana Lionel Dyck, mkurugenzi wa jeshi binafsi toka nchini Afrika Kusini, Dyck Advisory Group (DAG), ambayo inahusika na utoaji wa vifaa na wataalamu wa mapambano ya kivita.

photo_2020-07-16_13-24-27.png


Wanaweka makubaliano ya kupatikana kwa helikopta sita za vita na pia msaada wa anga kuwakabili magaidi.

Kwa muda huo 2020, hapo Msumbiji kulikuwa na helikopta moja tu ya combat, Russian-built MI-8, tena waliyopewa kama msaada na Rais Putin mwaka 2017.

EFYXrHGXkAA0LPC-768x1024.png


DAG wanaanza oparesheni yao April, 2020, wakikatiza anga la Msumbiji kupambana pembeni ya wanausalama.

images(17).jpg


Lakini misheni yao ikiwa imebakiwa na wiki mbili tu kumalizika, linatokea shambulizi la mji wa Palma.

Shambulizi kubwa la kigaidi kupata kutokea katika ukanda huu wa kusini mwa Afrika.

Watu takribani 1,200 - 1,400 wanauawa ndani ya siku moja. Maiti zinazagaa barabarani. Mamia ya watu, ikiwemo watoto, wanaokotwa wakiwa hawana vichwa.

7f11dcf905d2af2870a91cf643af8bc9.png


Shambulizi hizi linashtua jumuiya mataifa ya kusini mwa Afrika (SADC), na sasa linaazimia kufanya kitu upesi kabla hatujaipoteza nchi ya Msumbiji mazima.

5ccf64ce7a3f9d8a9a5786e76fa61ca7.png


Na Rwanda naye habaki nyuma. Anaingiza miguu yake eneo hili akidai kuisaidia Msumbiji kupambana na ugaidi ni njia mojawapo ya kujihakikishia usalama wake kama nchi.

97ea064b07be970af3e8db39bbd63c25.png


Lakini hana interests zingine hapa?

Kama hapana, je vile vikao vyake na raisi wa Msumbiji, Felipe Nyusi, pembeni ya mkurugenzi wa TotalEnergies, bwana Patrick Pouyannรฉ, vinatoa ujumbe gani?


Ikumbukwe shambulizi hili la mji Palma lilitokea karibu na mradi mkubwa wa dola 'mabilioni' ulio chini ya kampuni ya kifaransa ya TotalEnergies na kupelekea kampuni hiyo kufunga shughuli zake kwa muda usiojulikana.

pouyanne-kagame-scaled.jpg


Lakini yote kwa yote, Msumbiji imefikaje hapa? Intelijensia yake ililala wapi? Hawa magaidi ni kina nani na wanataka nini hapa Cabo Delgado?

Kuna mahusiano gani na mambo ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji)?

Habari inaanzia kule Mombasa, Kenya, miaka 12 ilopita...

๐“๐”๐๐†๐Ž๐‰๐„ ๐’๐„๐‡๐„๐Œ๐” ๐˜๐€ ๐Ÿฌ๐Ÿฎ:
 

Attachments

  • 957e775224010f55f3cc41b3d043edf3.png
    957e775224010f55f3cc41b3d043edf3.png
    268.8 KB · Views: 28
  • photo_2020-03-27_08-54-12.png
    photo_2020-03-27_08-54-12.png
    452.7 KB · Views: 19
  • Screenshot_20240528-213507.png
    Screenshot_20240528-213507.png
    878.8 KB · Views: 22
Tutafanyaje wakati hayo matendo kwa wengine ni njia ya kuiona pepo?

Bila hivyo wanaamini kwao hakuna kuiona pepo,na ktk situation kama hii ni rahisi sana watu kupaza sauti kwamba wanaonewa na kuchafuliwa kwa kufanya ibada zao tukichukulia nchi yetu tunaamini hakuna upendeleo wa kidini.
 
Back
Top Bottom