Njia rahisi ya kufanikiwa maishani.

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
Ili upate mafanikio ni lazima heshima iwe mbele.

Ili watu wakuheshimu ni lazima wewe mwenyewe kwanza ujiheshimu.
Ili ufikie mafanikio makubwa kwenye maisha yako ni lazima ujiheshimu.

Lakini watu wengi wamekuwa hawajiheshimu, na hii imekuwa inawazuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao.

Na kujiheshimu ninakozungumzia hapa hakuishii tu wewe kuwa mtu mwema na kuwa na maadili mazuri. Bali kunakwenda mbali zaidi mpaka kwenye mambo yako mengine binafsi.

Je unatekeleza mipango uliyojipangia? Kama umepanga kitu wewe mwenyewe, halafu unaacha kukitekeleza, kweli utasema unajiheshimu?
Kama muda ni wako mwenyewe, na unajua ni wa thamani, lakini bado unaupoteza, kweli unajiheshimu?

Una mke / mume halafu matatizo yenu ya ndani unayaanika kwenye mitandao ya kijamii, heshima ipo hapo?
Kama unajua uwezo wako ni mkubwa na unaweza kufanya zaidi ya unavyofanya sasa, lakini unaamua kufanya tu kawaida, kweli unajiheshimu?

Tafadhali sana, anza kufanya kile ambacho umepanga kufanya, anza kuongeza ubora ambao upo ndani yako, na utazidi kujiheshimu na wengine watakuheshimu zaidi.
Kuna watu huwa wanalalamika kwamba watu wenye hela wanaheshimika kuliko ambao hawana fedha.

Pamoja na sababu nyingine nyingi, moja wapo ni kujiheshimu.
Kuwa na fedha nyingi ni kielelezo kizuri cha kujiheshimu.

Hakuna mtu ambaye hajiheshimu, haheshimu mipango yake, haendi hatua ya ziada anayeweza kufikia utajiri.
Jiheshimu zaidi na utapata mafanikio makubwa sana.
Heshima si kuvaa vizuri, ila maisha unavyoishi.

Heshimu taaluma na watu walio kuzunguka.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…