Hahahaa, umenikumbusha babaangu baada ya kustaafu shirika la reli, akarudi kijijini, akakuta rafiki yake wa enzi za utoto ana biashara ya ng'ombe za minadani, basi yule mzee akamwambia ili aweze kumudu maisha ya kijijini aingie kwenye hiyo biashara yaani unanunua ng'ombe mnada huu leo kesho kutwa mnapeleka mnada mwingine.
Basi baba akashawishika, inaonyesha baada kuingia kwenye hii biashara ya uchuuzi wa ng'ombe akaona upungufu kwenye matumizi ya huyu mzee mwenzake ingawa alikuta ina faida.
Siku moja wakiwa nyumbani baba akaanza kumuuliza mswali ambayo huyo mzee hakuyapenda.
Swali: katika mtaji wako huwa unatumia % ngapi? Ukiwa, kwenye eneo la mnada?
Jibu: kwanza lazima nipate busia kopo moja na supu ya mbuzi ndipo naendelea na mengine.
Baba akamwambia waunganishe mtaji uwe moja,akakubali, siku ya mnada wakanunua ng'ombe, wakauza, waliporudi nyumbani wakaanza kupiga mahesabu ya mapato na matumizi.
Baba: figure yetu ni 100%.
Mzee: mambo ya wanawake tena ya nini? Tuongee mambo ya muhimu,mambo ya mafiga kwani tulienda kupika?
Baba: siyo hivyo ni hesabu hiyo we tulia utanielewa.
Mzee: sawa endelea.
Baba
rofit ni 19%.
Mzee: ehe!
Baba: matumizi.
Mzee: ndiyo.
Baba: ushuru 0.01%
Mzee: ndiyo nini?
Baba: kiwango cha profit kilichotumika.
Mzee: we bwana ... Hii biashara kila mtu achukue chake tutaharibu uhsiano wetu na hizo % zako.