Thabit Madai
Member
- Oct 8, 2024
- 52
- 138
-NJE YA BOX
Yanga wamehama uwanja wa Azam Complex, hii ni baada ya kipigo mara mbili mfululizo kutoka kwa Azam Fc na Tabora United.
Yanga hawajaweka wazi kwanini wamekimbia Chamazi ila kuna maswali tunaweza kujiuliza:-
A) Sababu za kiufundi ?
B) Sababu za nje ya Uwanja au
C) Sababu za kiuchumi?
Kama Sababu ni za kiufundi ndio maana wamefungwa mbona wamewahi kushinda hapo hapo...walimfunga Kmc,JKT bao tano hapo hapo Chamaz?
Kama uwanja ni mdogo pengine, huko walikoenda uwanja una ukubwa gani? Kwamba vipimo vya uwanja vilifanya goli likawa dogo Aziz Ki akashindwa kufunga penati?
Kama sababu ni za nje ya uwanja ni zipi hizo? Au ile video iliyosambaa ikihusisha uchomaji wa Sindano? Sidhani!
Au ni sababu za kiuchumi? Timu imeshindwa kulipia uwanja? Hii nayo sio kweli.
NADHANI...
Tumewekeza zaidi nje ya uwanja kuliko ndani ya uwanja
Mashabiki wanasema Azam Fc wanawahujumu...nadhani tatizo ni fikra za kichawi tu kwasababu mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa wazi kila mtu anaona!
Simba nao walihama Chamazi kwa sababu hizo hizo za kufikirika za nje ya uwanja...
Hii inaleta tafsiri kwamba ubingwa wetu unapatikana nje ya uwanja zaidi kuliko ndani ya uwanja ndio maana pale Azam Complex wakubwa wanakimbia...
Azam Complex wamefunga camera ili kuwaona watu wanaomwaga dawa kitu ambacho wakubwa hawataki
Azam Complex mpaka watu wa usafi ni watu makini ndio maana hawako tayari kuona camera zimezibwa na mabomba ya sindano kwenye changing rooms...wakubwa wanaona wanabanwa!
Hiki ndio kitu nachokiona zaidi kwenye hili sakata...
Ndio maana unaona hawa wanahama wengine wanachukia kwasababu tayari huyu aliehama muda mrefu aliko kuna uhuru hivyo alitaka mwenzie aendelee kubanwa ili apoteze ubingwa!
Ni uchawi tu...
✍️Sospeter Ilagila