Njano, Nyekundu na Kijani Kwenye Bendera

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
16,684
21,933
Inawezekan baadhi yetu hatujawahi kutambua kwamba kuna nchi nyingi sana za kiafrika hutumia rangi hizi za nyano, nyekundu na kijani kwenye bendera zao.

Nimeweza kuweka mifano michache hapa. Ironically rangi hizo pia ndizo zinaztumiwa na wafuasi wa Reggae. Je, kuna aliyewahi kujiuliza kwanini iwe rangi hizo?

Drapeau-Flag-bandeira-Flagge-bandera-Rasta-Bob-Marley-Dreadlock-Jamaica-F320.jpg


1678674157153.png

1678674214925.png

1678674279646.png

Nitaleta jibu baadaye, lakini hebu na wewe jaribu kutoa maelezo yako kuhusu rangi hizo.
 
Bendera mbili hapo hufanana sana

Bendera ya mali na Guinea

Wanajeshi hasa wale wasioenda shule wa nchi ya MALI na GUINEA bendera yao ya nchi husika inaweza kupandishwa nchi nyingine na wakaona bado nchi yao ipo huru kumbe wamevamiwa. And vice versa.

Hata watoto shuleni huweza kuchora bendera ya Mali kumbe waliikusudia ya Guinea
 
Fafanua mkuu
Oooh wayback 2003 hizo ma rangi zilikua swaggar sana hasa ni vile rasta color na kuhusishwa na Mjani na kipindi hiyo tunamoka tunavuta zaidi ya oxygen, na kuwa na hizo bendera, deleki, bosholi, nk za hizo color kuonesha rastafarian na ukush,so nowadays hizo color zinahusishwa na mambo ya kiwaki.
 
Kwa kifupi ninavyoelewa, inasemekana kuwa wakati mataifa mengine ya Kiafrika yalipopata uhuru baada ya WWII, mengi kati yao yalichukua rangi za bendera ya Ethiopia, ambayo ilikuwa haijawahi kutawaliwa. Nchi hiyo ilivutia mataifa mengi mapya ya Afrika na mji mkuu wake Addis Ababa ukawa makao makuu ya mashirika na jumuiya za Kiafrika.

Ufalme wa Ethiopia (Ethiopian Empire) ulitumia rangi hizo katika bendera yake. Hata baada ya utawala wa kifalme kuisha, Ethiopia imekuwa ikitumia rangi hizo na imekuwa ikitafsiri rangi hizo hivi: Kijani inawakilisha utajiri na rutuba ya ardhi yao; Njano inawakilisha matumaini, na Nyekundu inawakilisha kujitoa kwa wananchi wake ambao walimwaga damu yao katika kulinda uhuru wa Ethiopia.

Ukichunguza utagundua kuwa rangi hizo zinabeba tafsiri kama hizo au zinazokaribiana na hizo kwa mataifa mengine ya Afrika yanayozitumia katika bendera zao.

Kijani, njano na nyekundu pia zimekuwa zikitumika kuwakilisha itikadi ya Umajumui wa Afrika (Pan-African ideology). Rastafari, kwa mfano, wanatumia rangi hizo wakizihusisha na Uafrika. Bendera wanayotumia Rastafari ni ile iliyokuwa ikitumika na Ufalme wa Ethiopia kuanzia miaka ya 1870s hadi 1974 ambayo inabeba picha ya Simba wa Yuda (Lion of Judah) ambayo ni nembo ya kitamaduni ya Kiyahudi.

Rasta wanaamini kwenye uhusiano wa mtu mweusi na Ethiopia. Kwa wengi ni Nchi ya ahadi.

Wakati Haile Selassie alipotoa ardhi huko Shashamane ili Waafrika walio utumwani warudi kwenye ardhi yao, si Rastafari pekee waliolengwa, lakini waliishia kuwa kundi kubwa zaidi la watu waliohama kutoka Jamaica na nchi zingine kwenda Shashamane. Harakati za kwanza za Rastafari kwenda Shashamane zilianza mwishoni mwa miaka ya 60 na katikati ya miaka ya 70.
 
Haya kwakukusaidia tu ni kuwa hata Tanzania tuna kijani na njano tofauti hatuna nyekundu kwakua inasemekana rangi hiyo hutumiwa na waliopata uhuru Kwa arms struggle.

Kuhusisha rangi hizo na kampeni yenu yakupigia chapuo swala lenu ni matumizi mabaya ya ubongo.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hiyo sentensi niliyowekea rangi imeandikwa bila kutumia busara yoyote, ni ya aina ya watu waropokaji.

Rangi nyekundu haina maana ya vita. Kuna nchi nyingi zenye rangi nyekundu kwenye bendera zao lakini ama hazikuwahi kutawaliwa kabisa, kwa mfano Uingereza, Ufaransa, Italy, Urusi na Japan ama hazikupigana vita ili kupata uhuru wao kwa mfano Canada, Australia na New Zealand.

Kwa hiyo acha kuandika mambo kwa kuhisia bila kuwa na uhakika.
 
Back
Top Bottom