Njaa inakuja, Serikali CCM imejiandaaje???

Determinantor

Platinum Member
Mar 17, 2008
57,754
92,178
Wakuu
Kwanza kwa kimya cha dakika moja natulia ili kumkumbuka Memba mwenzetu dena ambaye amemaliza kazi yake, bado Mimi na Wewe. Amen


Mvua hakuna, mahindi yamekufa na mimea mingine ya chakula! Ni wazi hali si shwari na mvua chache sana zinazonyesha ni kwamba zinamaliza kabisa mahindi na mazao madogo yaliyopandwa. Sio siasa ni facts!

Je serikali imejiandaaje??? Je kuna akiba ya kutosheleza mahitaji kwa kipindi hiki kigumu mbele yetu??? Ombi langu tusije tukaweka siasa kama kule Kagera, haya ni maisha yetu sote. Yale yaliyotokea yawe funzo.

Kwa viongozi wote, kama kuna njaa sema ukweli japo utawagharimu lakini tutawakumbuka siku moja. Najua wengi wataenguliwa kwa kutangaza njaa kwenye maeneo yao! Chagueni fungu jema.
 
Hii njaa haiko mbali soon tutaanza kuiexperience, bei ya debe moja la mahindi kwa sasa ina rank 15000, kwa ukosefu huu wa mvua tutegemee makubwa mwakan miez ya mwanzo, hali ni tete kwa kweli
 
Juzi nimenunua kiloba cha sembe kilo 25 kwa bei ya shilingi 35000,muuzaji ananiambia inapoelekea itafikia mpaka 40 elfu,Jamani serikali acheni siasa semeni ukweli tu kuhusu hili balaa la njaa
 
wallah, njaa inakuja tena kali sana, na kama mvua hazijanyesha, kwa kweli njaa kali sana inakuja, nilienda ukerewe nimekaa wiki 3 hali ni mbaya sana, jua mwanzo mwisho, mimea imekauka, mvua hakuna, aisee kama mvua ikikosa kunyesha kipindi hiki njaa kubwa sana inakuja, sasa serikali sijui imejipangaje, manake watu hawana namna, wameshachekecha vichwa lakini hawajapata njia mbadala, watu wanashindia maembe, na msimu wa maembe unaondoka sasa,
 
Tarime huko imeshafika 22,000
Ni kweli mkuu...hiyo ndo bei ya hapa..

kasuku moja ni 2200/2300 .


sasa ukinunua debe(kasuku 10) ni22000.

Halafu ni shida sana kupata mahindi ya kununua..
walah Mwenyezi Mungu atunusuru na hii njaa inayotunyemelea
 
Sijui waziri wa kilimo nani maana naona kalala fofofo,bora wangemwaacha mwigulu angeshatoa way forward.

Inatakiwa waanze kuandaa kufungua akiba ya mahindi,
kwa mtu wa hali ya chini bei ya mahindi iko juu mno
 
Sijui waziri wa kilimo nani maana naona kalala fofofo,bora wangemwaacha mwigulu angeshatoa way forward.

Inatakiwa waanze kuandaa kufungua akiba ya mahindi,
kwa mtu wa hali ya chini bei ya mahindi iko juu mno
Bahati nzuri hata siwafahamu Aisee Mawaziri hata mmoja!!!! Hali ni mbaya mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…