Hata humu JF watu tumrathirika na njaa.Kama Kilo 1 ya unga ilikuwa ikiuzwa 1,000/- saivi inauzwa 1,600/- unaweza kusemaje wanaJF hatujaathirika.Kama tuna ndugu zetu ,wazazi wetu huko vijijini wanategemea kilimo cha mvua wameathirika unawezaje kusema wanaJF hatujaathirika?? Kwa kuathirika ndugu zetu huko maana yeke sisi tunaotegemewa tuongeze msaada mara dufu ili kuokoa jahazi.
Serikali ni lazima ilaumiwe kwa kuwa inashindwa kutambua vipaumbele vya msingi.Pesa waliyonunulia ndege hizo mbili zingetumika kutengeneza irrigation schemes maelfu ya watanzania wangeweza kuzalisha kwa manufaa ya mamilioni ya watanzania.