Niwe na Imani ipi juu ya Hili tatizo??

SIRE

Senior Member
Feb 20, 2022
112
162
Ndugu wa JF, Nawasalimu wote.

Bila kupoteza wakati nianze kwa kutoa maelezo mafupi ya kile kinachomsibu ndugu yangu wa karibu sana jambo ambalo linaniathiri na mimi pia.

Nina huyo mamdogo wangu ambaye ni kama mama yangu kutokana na namna nzuri alivyonisaidia kunisapoti kimasomo wakati niko shuleni.

Amebahatika kuwa na nzao mbili lakini ameshindwa kushika ujauzito wa tatu baada ya mimba kuharibika. Imani yake kubwa ni kuwa amerogwa ambapo analalamika kuwa pengine amerushiwa nguvu za Giza zinazomfanya asikamate mimba.

Nimejaribu kumfuatilia kwa maelezo yake ni kuwa "kuna kitu kigumu kwenye tumbo lake kuanzia kwenye kitovu kupanda juu ambapo Huwa kina kinadunda mithili ya mapigo ya moyo na pia Huwa ni kama kinapumua kwa kuendana na upumuaji wake."

Amejaribu kuzunguka kwa wataalamu Ili kupata ufumbuzi lakini hakujazaa matunda. Pia alishwahi kufanya check up za ultrasound pia haikuwa na matunda.

Kutokana na maelezo yake na jinsi nilivyong'amua huyu mama yangu ana shida ya hospitali zaidi. Na pengine ni hernia za wakina mama.

Nimeliletwa kwenu mnisaidie kimawazo Ili nipate namna njema ya kumshauri maana naona ameshapaniki na anaona kama ametengwa kutokana na kukosa wa kumshauri.

Ahsanteni Sana.
 
Ni uvimbe huo,au tezi kwenye kizazi
Unadhani watu Wana muda wa kuroga sikuhizi...wapo busy habari za Balt...
Yote Tisa,ameshindwa kujiuliza kwanini wasingemroga kabla hajapata hata hao watoto wengine
 
Dawa ya kwanza kabisa, Aondoe hofu ya kwamba amerogwa.
Matatizo ya uzazi yapo mengi.
Pengine Baada ya mtoto wa 2 alitumia uzazi wa mpango kitu kinachoweza kusababisha hitlaf ndogondogo ambazo zinahitaji ushauri wa kitaalam zaidi kuliko kutanguliza urooogii mbele.

Ivo tuu aani mengine wengine chini huko.
 
Pole sana.
Tatizo la kutoshika mimba (infertility) lipo na linatibika hasa baada ya kubaini kisababishi chake.

Kwa hiyo mshauri aende hospitali aonane na daktari bingwa wa kina mama na uzazi (obstetrician and gynecologist) ili afanyiwe uchunguzi na vipimo hatimaye kupata matibabu sahihi.
Kila lakheri.
 
Ni uvimbe huo,au tezi kwenye kizazi
Unadhani watu Wana muda wa kuroga sikuhizi...wapo busy habari za Balt...
Yote Tisa,ameshindwa kujiuliza kwanini wasingemroga kabla hajapata hata hao watoto wengine
Shukrani kwa ushauri
 
Dawa ya kwanza kabisa, Aondoe hofu ya kwamba amerogwa.
Matatizo ya uzazi yapo mengi.
Pengine Baada ya mtoto wa 2 alitumia uzazi wa mpango kitu kinachoweza kusababisha hitlaf ndogondogo ambazo zinahitaji ushauri wa kitaalam zaidi kuliko kutanguliza urooogii mbele.

Ivo tuu aani mengine wengine chini huko.
Sina hakika sana mkuu.
 
Back
Top Bottom