Niulize chochote kuhusu homa ya ini. Kiufupi homa ya ini ni ugonjwa unaosabishwa na virusi aina ya 'Hepatitis A, B, C, D & E). Maswali yanaweza kujikita kwenye B na C kutokana kupelekea kusababisha saratani ya ini(Hepatocellular carcinoma). Mpaka sasa 'Hep B' haina tiba kamili ya kuiondoa, hivyo, matibabu yamejikita kwenye kufubaza virusi(kama ilivyo HIV) kwa 'Antiviral medications' kupunguza athari kwenye ini. Kwa upande mwingine 'Hep C' inatibika na huweza kutoweka kabisa. Ifahamike ugunduzi wa mapema na kuanza dawa na muhimu sana kwani ini likifikia hatua ya saratani hata kama utatibu 'Hep C' bado tatizo litaendelea.