Niulize chochote kuhusiana na ugonjwa wa homa ya ini

MAMDALI

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
219
434
Niulize chochote kuhusu homa ya ini. Kiufupi homa ya ini ni ugonjwa unaosabishwa na virusi aina ya 'Hepatitis A, B, C, D & E). Maswali yanaweza kujikita kwenye B na C kutokana kupelekea kusababisha saratani ya ini(Hepatocellular carcinoma). Mpaka sasa 'Hep B' haina tiba kamili ya kuiondoa, hivyo, matibabu yamejikita kwenye kufubaza virusi(kama ilivyo HIV) kwa 'Antiviral medications' kupunguza athari kwenye ini. Kwa upande mwingine 'Hep C' inatibika na huweza kutoweka kabisa. Ifahamike ugunduzi wa mapema na kuanza dawa na muhimu sana kwani ini likifikia hatua ya saratani hata kama utatibu 'Hep C' bado tatizo litaendelea.
 
Je ni ugonjwa wa kuambukizwa?
Jibu ni Ndiyo.
Maelezo; Virusi vya ini aina ya 'B' na 'C' vinaambukiza kwa njia mbalimbali; B; kujamiana na mtu mwenye maambukizi, kushiriakiana vitu vyenye ncha kali na mtu mwenye maambukizi, michubuko, 'tattoo' n.k. kwa 'C'; Kuongezewa damu isiyo salama yenye maambukizi ya virusi-Hep C, na nyinginezo kama kujamiana n.k.

Kama ikitokea mwenza wako(au mshiriki wa ngono) ana aina ya B au C hunabudi kupima na ikiwa itaonekana huna maambukizi (Discondant couple) basi kama mwenza wako alionekana na homa ya ini aina ya 'B' basi utatakiwa upate chanjo. Sambamba na hilo kama una wanafamilia ambao mnaishi pamoja na muathirika ni muhimu wote kupima na kupata chanjo. Kwa upande wa 'C' haina chanjo mpaka sasa ila inatibika.
 
Kwa upande wa homa ya ini sio watu wote wanaopata B au C basi hupelekea kuwa na virusi daima hapana. Tafiti zinasema; Kwa upande wa aina ya 'B' kwa watu wazima(healthy adults) ambao wamepata maambukizi; asilimia 95 mpaka 99 kinga mwili huweza kuvishambulia 🦠 na kuviondoa ndani ya miezi sita(acute hepatitis B 🦠), ni asilimia 5 pekee huenda kuwa na 🦠 kwa muda wote(chronic hepatitis B 🦠)-baada ya miezi sita. Kati asilimia 5 ya watu wenye 'chronic hepatitis B virus ->asilimia 8 mpaka 20 hupelekea ini kusinyaa(liver cirrhosis) ndani ya miaka mitano. Athari ya kupata saratani ya ini kwa mtu mwenye 'chronic hepatitis B' ni kati ya asilimia 1 mpaka 5 kwa mwaka. Kwa upande wa Hepatitis C ni tofauti kidogo
 
Back
Top Bottom