Niuanze uandishi wa vitabu lini?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
7,190
10,316
Perfectionism na kuwa "media shy" ni miongoni mwa vizuizi ambavyo ningali ninakabiliana nazo. Naelezea:

PERFECTIONISM
Najiona bado sijakidhi vigezo vya kiunadishi. Japo lengo langu kuu si kujipatia fedha bali kuufikisha ujumbe kwa hadhira lengwa, sipendi kufanya jambo ambalo sijashawishika kuwa litawanufaisha walengwa.

Sipendi, kwa mfano, mtu asome kitabu nitakachokiandika na asinufaike nacho. Nataka kila akisomaye apate alau "wazo" litakalomsaidia, au aburidike, alau.

Najiona ningali na changamoto ya kupangilia "point" kwa usahihi, na wakati mwingine, huwa ninasumbuka sana kuweza kuufikisha ujumbe kwa njia ya maandishi, ingawa kuwasilisha ujumbe kwa maandishi ni njia bora zaidi kwangu kuliko kwa kuongea.

MEDIA SHY
Naweza kusema mimi ni "media shy" kwa kiasi fulani. Siupendi "umaarufu".

Endapo vitabu vyangu vitapendwa, vitaweza kusambaa sehemu mbalimbali nchini. Naona kama ni kero ikiwa karibia kila nitakakokwenda nitakuwa nafahamika.

Nimekuwa nikifikiria niandike lakini kwenye jina la mtunzi niliweke jina la mtu mwingine, kwamba, nisilitumie jina langu halisi, japo sijajua kama hilo linawezekana.

Nini ushauri wako kuhusiana na hizo changamoto?

Ni zaidi ya miaka kumi sasa nikiwa ninasitasita kuanza uandishi. Miaka ya nyuma , nilianza kwa kuandika sura mbili, lakini niliamua kusitisha hadi muda "muafaka". Mpaka sasa, sura mbili nilizoziandika zingali kwenye faili zikisubiria sura zingine za kuikamilisha kitabu.

Miaka kadhaa iliyopita, niliweka malengo kuwa ifikapo Jumapili ya tarehe 14 May... nitasherekea kutimia kwa malengo yangu ya miaka kumi. Miongoni mwa hayo malengo ni kukamilisha uandishi wa zaidi ya vitabu kumi. Ni miaka michache tu ndiyo imesalia ilhali sijatoa hata kitabu kimoja.

Nifanyeje?
 
Hebu jaribu kwanza hapa JF Stories of Change tuone uwezo wako, ila kwa hizo 'alau alau' zinatia mashaka kwenye uandishi wako.
 
Hebu jaribu kwanza hapa JF Stories of Change tuone uwezo wako, ila kwa hizo 'alau alau' zinatia mashaka kwenye uandishi wako.
Bora yako wewe ni leo ndiyo unauonea mashaka uandishi wangu. Mimi nimekuwa katika mashaka kwa zaidi ya miaka kumi. Ndiyo maana nimeendelea kusita mpaka sasa.
 
Bora yako wewe ni leo ndiyo unauonea mashaka uandishi wangu. Mimi nimekuwa katika mashaka kwa zaidi ya miaka kumi. Ndiyo maana nimeendelea kusita mpaka sasa.
Uzuri wa uandishi wa vitabu huwa kuna wahariri, watakusaidia kuondoa hizo changamoto ndogo ndogo.... kusitasita sasa kufike mwisho.
 
Back
Top Bottom