Nitamshangaa sana Nape kama hatachukua hatua za haraka kwenye hili

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,309
3,337
Labda mtu anipe tafsiri tofauti ya neno uchochezi ni nini lakini vinginevyo hili gazeti lazima lichukuliwe hatua.

Kuandika kwamba watanzania wanakosa imani na raisi si sawa kwani huweza kupelekea ama kujenga taswira hasi ama kuleta hofu zisizo za kweli ama kwa rais ama kwa watanzania.

Ni vema vyombo vya habari vikawa makini kuchuja habari zake ili zisilete taharuki na kulinda amani tulionayo kwani vyombo vya habari vina nguvu mno aidha kuchafua ama kuilinda hii amani tulionayo

Kuna kila sababu Nape akachkua hatua harakaharaka ili kudhibiti hiii hali isiendelee.

Up to date
Hizi comment zote hapa chini zinazosema "hata mimi sina imani naye" ni zao la uchochezi wa hili gazeti mbona kabla hamkusema?
Nape chukua hatua haraka.
 
Hata akifungua kesi mahakamani atashindwa, nini maana ya vyombo vya habari?
Wao wanareport mambo yanayoendelea bila upendeleo, kama wananchi hawana imani na Rais then so be it, ndio ukweli utatangazwa, unless kama inaweza kua proved kua data hizo wamejitungia wenyewe, ila hata kama ni survey ambayo imehusisha watu 500 inatosha kabisa kua published.
 
The problem wananchi tunadhani haya yanayolalamikiwa na wengine sisi hayatuhusu au hayawezi kutupata! Ajabu hao hao wakipigwa ban na JF utakuta wanalalamika huku wakisahau kwamba, tukiendelea kushangilia upumbavu kuna siku utakuja kuambiwa social media zote zimefungiwa!
 
Labda mtu anipe tafsiri tofauti ya neno uchochezi ni nini lakini vinginevyo hili gazeti lazima lichukulowe hatua.

Kuandika kwamba watanzania wanakosa imani na raisi si sawa kwani huweza kupelekea ama kujenge taswira hasi ama kuleta hofu zisizo za kweli kwa raisi.

Ni vema vyombo vya habari vikawa makini kuchuja habari zake ili zisilete taharuki na kulinda amani tulionayo kwani vyombo vya habari vina nguvu mno aidha kuchafua ama kuilinda hii amani tulionayo

Kuna kila sababu Nape akachkua hatua harakaharaka ili kudhibiti hiii hali isiendelee.
juzi nilileta uzi hapa nikawaambia kuwa kuna jamii fulani wa chama fulani wanaamini jpm atapinduliwa kabla ya 2020 na mapinduzi hayo wao wanaamini yatatokea soon. gazeti kama hili ni la hao hao watu wa jamii hiyo wa chama hicho
 
Sheria namba 9 ya Takwimu ya mwaka 2015 ambayo katika kifungu cha 37(3) kimeainisha makosa na adhabu kuwa ni pamoja na vyombo vya habari kuleta takwimu za upotoshaji.

Nachojiuluza ni je, taarifa ya kiutafiti ya gazeti la JamboLeo kuhusu kukubaliki kwa Rais Magufuli hakuhusiana na sheria hii?

Nafahamu si kila tafiti zinabanwa na hii sheria kwa mfano zile za wanafunzi wa vyuo vikuu, n.k

Lakini je,tafiti hizi zinazohusu vyombo vya habari ziko huru kiasi hiki?

Kama nakumbuka sawaswa, adhabu yake huwa ni kifungo kisichopungua miezi 6 jela au faini isiyopungua shilingi milioni moja.

Gazeti limefanya kazi yake, lakini je,litasalimika?

Swali muhimu kuliko yote hapa ni je,gazeti hili limepata ruhusu ya National Bureau of Statistics(NBS) kabla ya kuchapisha habari hii?
 
Haiwezekani watu na hang over zao za kushindwa uchaguzi mkuu na kubanwa waache ufisadi ikageuka chuki na njia ya kumfitinisha raisi na wananchi. Hili haliwezekani na naamini kichapo kwa wamiliki wa hili gazeti lazima kitumwe, na ikiwezekana wachunguzwe zaidi hawa watu
 
Kumbe kinachogombewa na UKUTA kina hoja,na yaliyosemwa na Lissu ni kweli!!!Kwa awamu hii ukweli ni uchochezi
 
umejishaua weeee,haya hofu zilizo za kweli ni zipi sasa!!!mbona mnapanic?
 
Back
Top Bottom