Nitabaki na mke wangu na wanangu, kumbe ndugu ni kenge tu

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,302
2,020
KUNA WATU HAWANA SONI ILA NITAWAFURAHISHA, MNAJIITA NDUGU ZANGU KUMBE NI KENG*E TU!

Kama unavyojua familia za Kiafrika, mmoja akishatoka kimaisha basi unachagua na ndugu zako kuja kuwasaidia. Hiyo ndiyo ilikuwa kwangu, nilihangaika na maisha ya ndugu zangu mpaka wote wakamaliza chuo.

Bila mkopo nilisomesha wadogo zangu wanne, wamemaliza chuo suala la ajira sasa nikawa sina namna, sina connection, hawana kazi ila kila mmoja anahangaika na maisha yake mjini na mimi nikasema nahangaika na yangu.

Nimejitahidi nimejenga kanyumba kangu na kununua kausafiri kangu. Vyote hivi nafanya na mke wangu, yeye anafanya biashara mimi ni muajiriwa, hata pesa ya kuwasomesha kiasi kikubwa ilikuwa inatoka kwenye biashara yaani ni kama mke wangu ndiyo alisomesha ndugu zangu.

Si biashara kubwa ila imesaidia, mwaka jana mwezi wa tisa nilianza kuumwa, niliumwa sana nimelazwa hospitalini kuanzia mwezi wa tisa mpaka mwezi wa kumi na mbili.

Kila kitu nafanyiwa sijitambui, mke wangu alihangaika sana, ndugu mwanzo walikuwa na mimi lakini mwishoni alibaki mke wangu peke yake. Kutokana na kuhangaika na mimi ilibidi watoto kuwapeleka kwao.

Kumbuka nina ndugu zangu hapa Dar, maisha najua ni magumu lakini wangekuwa wameshindwa kuishi na watoto wangu hakuna mtu anataka kabisa, ila ndiyo hivyo kila mmoja alikuwa bize na kazi zake, mara sina mfanyakazi, mara sijui nini basi ikawa hivyo.

Nimetoka hospitalini nikiwa bado na hali mbaya, sema ni ile nimerudishwa tu, nadhani ni kama unaambiwa kafi*e nyumbani. Nimerudi mke anahangaika, mara dukani mara kuniuguza. Mara napata nafuu nashangaa ndugu wanakuja sasa, wanakuwa karibu.

Ni kama walikuwa hawaamini kuwa nitapona. Basi mimi nikawa sina shida ndiyo maisha, kama mwanaume unajua kuwa kupambana ni wewe na mke wako. Basi juzi wakati sasa naangalia vitu vyangu nakuta hati ya nyumba siioni.

Namuuliza mke wangu ananiambia hajui, kadi ya gari sioni, mke wangu ananiambia sijui. Nilipaniki sana nikahisi kuna binti wa kazi aliyekuwepo akaondoka nikajua ni yeye. Basi nikampigia simu kumuuliza, aisee nilichosikia!

Ananiambia mbona Shangazi, alikuja nyumbani na kuchukua kila kitu wakasema wanahifadhi kwa kuwa Mama anaweza kuondoka navyo. Kwa maana ya dada yangu mkubwa, ana ndoa yake, wamekuja na ndugu wengine, wakaingia mpaka chumbani kwangu.

Mke wangu yuko hospitalini eti nikif*a hawatapata kitu mke wangu anaweza kuvificha! Aisee, hasira nilizopata nikiangalia hata sijaka sawa wanangu hawana pa kukaa, aisee! Mke wangu kaingia madeni tena kwa ndugu zake hawa mbuzi wanawaza mali zangu!

Namfuata dada namuambia kuhusu vitu vyangu anajiuma uma, aisee nilichukua pang*a, nikamuangalia jicho moja alitoa kila kitu!

Halafu hawa Mbuzi wasio na akili sasa hivi wanatangaza mke wangu ndiyo kaniloga ndiyo maana nimekuwa makali, naomba uandike hapa wanakusoma waambie waache kuhangaika na maisha yangu maana nitawafurahisha kama wakitaka kumfanya chochote huyu mwanamke!

Nishamaliza nimejua rangi zenu! Yaani haka kanyumba ndiyo mnataka kuhangaika, dada hata kukaa na wanangu tu ili mke wangu ahanagike na hospitali ni shida wakati mtoto wako aliumwa nusu kuf*a mpaka nikauza pikipiki yangu ili apone, nasikitika Mungu nitakuwa sawa ila jueni tu kuwa haitakuwa sawa tena!
1690266300401.jpg
 
KUNA WATU HAWANA SONI ILA NITAWAFURAHISHA, MNAJIITA NDUGU ZANGU KUMBE NI KENG*E TU!

Kama unavyojua familia za Kiafrika, mmoja akishatoka kimaisha basi unachagua na ndugu zako kuja kuwasaidia. Hiyo ndiyo ilikuwa kwangu, nilihangaika na maisha ya ndugu zangu mpaka wote wakamaliza chuo.

Bila mkopo nilisomesha wadogo zangu wanne, wamemaliza chuo suala la ajira sasa nikawa sina namna, sina connection, hawana kazi ila kila mmoja anahangaika na maisha yake mjini na mimi nikasema nahangaika na yangu.

Nimejitahidi nimejenga kanyumba kangu na kununua kausafiri kangu. Vyote hivi nafanya na mke wangu, yeye anafanya biashara mimi ni muajiriwa, hata pesa ya kuwasomesha kiasi kikubwa ilikuwa inatoka kwenye biashara yaani ni kama mke wangu ndiyo alisomesha ndugu zangu.

Si biashara kubwa ila imesaidia, mwaka jana mwezi wa tisa nilianza kuumwa, niliumwa sana nimelazwa hospitalini kuanzia mwezi wa tisa mpaka mwezi wa kumi na mbili.

Kila kitu nafanyiwa sijitambui, mke wangu alihangaika sana, ndugu mwanzo walikuwa na mimi lakini mwishoni alibaki mke wangu peke yake. Kutokana na kuhangaika na mimi ilibidi watoto kuwapeleka kwao.

Kumbuka nina ndugu zangu hapa Dar, maisha najua ni magumu lakini wangekuwa wameshindwa kuishi na watoto wangu hakuna mtu anataka kabisa, ila ndiyo hivyo kila mmoja alikuwa bize na kazi zake, mara sina mfanyakazi, mara sijui nini basi ikawa hivyo.

Nimetoka hospitalini nikiwa bado na hali mbaya, sema ni ile nimerudishwa tu, nadhani ni kama unaambiwa kafi*e nyumbani. Nimerudi mke anahangaika, mara dukani mara kuniuguza. Mara napata nafuu nashangaa ndugu wanakuja sasa, wanakuwa karibu.

Ni kama walikuwa hawaamini kuwa nitapona. Basi mimi nikawa sina shida ndiyo maisha, kama mwanaume unajua kuwa kupambana ni wewe na mke wako. Basi juzi wakati sasa naangalia vitu vyangu nakuta hati ya nyumba siioni.

Namuuliza mke wangu ananiambia hajui, kadi ya gari sioni, mke wangu ananiambia sijui. Nilipaniki sana nikahisi kuna binti wa kazi aliyekuwepo akaondoka nikajua ni yeye. Basi nikampigia simu kumuuliza, aisee nilichosikia!

Ananiambia mbona Shangazi, alikuja nyumbani na kuchukua kila kitu wakasema wanahifadhi kwa kuwa Mama anaweza kuondoka navyo. Kwa maana ya dada yangu mkubwa, ana ndoa yake, wamekuja na ndugu wengine, wakaingia mpaka chumbani kwangu.

Mke wangu yuko hospitalini eti nikif*a hawatapata kitu mke wangu anaweza kuvificha! Aisee, hasira nilizopata nikiangalia hata sijaka sawa wanangu hawana pa kukaa, aisee! Mke wangu kaingia madeni tena kwa ndugu zake hawa mbuzi wanawaza mali zangu!

Namfuata dada namuambia kuhusu vitu vyangu anajiuma uma, aisee nilichukua pang*a, nikamuangalia jicho moja alitoa kila kitu!

Halafu hawa Mbuzi wasio na akili sasa hivi wanatangaza mke wangu ndiyo kaniloga ndiyo maana nimekuwa makali, naomba uandike hapa wanakusoma waambie waache kuhangaika na maisha yangu maana nitawafurahisha kama wakitaka kumfanya chochote huyu mwanamke!

Nishamaliza nimejua rangi zenu! Yaani haka kanyumba ndiyo mnataka kuhangaika, dada hata kukaa na wanangu tu ili mke wangu ahanagike na hospitali ni shida wakati mtoto wako aliumwa nusu kuf*a mpaka nikauza pikipiki yangu ili apone, nasikitika Mungu nitakuwa sawa ila jueni tu kuwa haitakuwa sawa tena!View attachment 2862305
 
KIkubwa Balance Maisha,Pigania kuweka misingi sawa.
1.Mali tafuta Mwanasheria wako,tuache kuishi simple simple,Elekeza mali.zako.wapi ziende kama ukikata moto ghafla.

2.Kama Mkeo amekupigania kiasi hicho endeleza Upendo mkuu kwake kwa kuangalia nini unamfanyia ili siku ukikata Moto ghafla watoto hawatopelekwa kwa ndugu.

3. Tambua sio katika ndugu zako wote ni wakola kuna mmoja au wawili waweza kuahikamana nao.Duniani hapa life ni unafiki tu..ndio Binadamu tumeumbwa.

4.Tujifunze kuwa na vitega uchumi,hata ukiumwa ghafla usiteteleke.

5.Kuna baadhi ya marafiki wako na moyo wa Kiskauti sana zaidi ya ndugu,ni sisi tu kuamua kuwachambua vyema kwa Rehema za Mwenyazi Mungu.

Tumepitia haya maisha na tuko nayo.Akili itulize sana mwana.

Visa tunavyo vingi sana sana..
 
KUNA WATU HAWANA SONI ILA NITAWAFURAHISHA, MNAJIITA NDUGU ZANGU KUMBE NI KENG*E TU!

Kama unavyojua familia za Kiafrika, mmoja akishatoka kimaisha basi unachagua na ndugu zako kuja kuwasaidia. Hiyo ndiyo ilikuwa kwangu, nilihangaika na maisha ya ndugu zangu mpaka wote wakamaliza chuo.

Bila mkopo nilisomesha wadogo zangu wanne, wamemaliza chuo suala la ajira sasa nikawa sina namna, sina connection, hawana kazi ila kila mmoja anahangaika na maisha yake mjini na mimi nikasema nahangaika na yangu.

Nimejitahidi nimejenga kanyumba kangu na kununua kausafiri kangu. Vyote hivi nafanya na mke wangu, yeye anafanya biashara mimi ni muajiriwa, hata pesa ya kuwasomesha kiasi kikubwa ilikuwa inatoka kwenye biashara yaani ni kama mke wangu ndiyo alisomesha ndugu zangu.

Si biashara kubwa ila imesaidia, mwaka jana mwezi wa tisa nilianza kuumwa, niliumwa sana nimelazwa hospitalini kuanzia mwezi wa tisa mpaka mwezi wa kumi na mbili.

Kila kitu nafanyiwa sijitambui, mke wangu alihangaika sana, ndugu mwanzo walikuwa na mimi lakini mwishoni alibaki mke wangu peke yake. Kutokana na kuhangaika na mimi ilibidi watoto kuwapeleka kwao.

Kumbuka nina ndugu zangu hapa Dar, maisha najua ni magumu lakini wangekuwa wameshindwa kuishi na watoto wangu hakuna mtu anataka kabisa, ila ndiyo hivyo kila mmoja alikuwa bize na kazi zake, mara sina mfanyakazi, mara sijui nini basi ikawa hivyo.

Nimetoka hospitalini nikiwa bado na hali mbaya, sema ni ile nimerudishwa tu, nadhani ni kama unaambiwa kafi*e nyumbani. Nimerudi mke anahangaika, mara dukani mara kuniuguza. Mara napata nafuu nashangaa ndugu wanakuja sasa, wanakuwa karibu.

Ni kama walikuwa hawaamini kuwa nitapona. Basi mimi nikawa sina shida ndiyo maisha, kama mwanaume unajua kuwa kupambana ni wewe na mke wako. Basi juzi wakati sasa naangalia vitu vyangu nakuta hati ya nyumba siioni.

Namuuliza mke wangu ananiambia hajui, kadi ya gari sioni, mke wangu ananiambia sijui. Nilipaniki sana nikahisi kuna binti wa kazi aliyekuwepo akaondoka nikajua ni yeye. Basi nikampigia simu kumuuliza, aisee nilichosikia!

Ananiambia mbona Shangazi, alikuja nyumbani na kuchukua kila kitu wakasema wanahifadhi kwa kuwa Mama anaweza kuondoka navyo. Kwa maana ya dada yangu mkubwa, ana ndoa yake, wamekuja na ndugu wengine, wakaingia mpaka chumbani kwangu.

Mke wangu yuko hospitalini eti nikif*a hawatapata kitu mke wangu anaweza kuvificha! Aisee, hasira nilizopata nikiangalia hata sijaka sawa wanangu hawana pa kukaa, aisee! Mke wangu kaingia madeni tena kwa ndugu zake hawa mbuzi wanawaza mali zangu!

Namfuata dada namuambia kuhusu vitu vyangu anajiuma uma, aisee nilichukua pang*a, nikamuangalia jicho moja alitoa kila kitu!

Halafu hawa Mbuzi wasio na akili sasa hivi wanatangaza mke wangu ndiyo kaniloga ndiyo maana nimekuwa makali, naomba uandike hapa wanakusoma waambie waache kuhangaika na maisha yangu maana nitawafurahisha kama wakitaka kumfanya chochote huyu mwanamke!

Nishamaliza nimejua rangi zenu! Yaani haka kanyumba ndiyo mnataka kuhangaika, dada hata kukaa na wanangu tu ili mke wangu ahanagike na hospitali ni shida wakati mtoto wako aliumwa nusu kuf*a mpaka nikauza pikipiki yangu ili apone, nasikitika Mungu nitakuwa sawa ila jueni tu kuwa haitakuwa sawa tena!View attachment 2862305
Kumbuka.

Wahenga walisema maneno mengine yenye maana ukiyaunganisha na habari yako.

1. Tenda wema, nenda zako. Usingoje shukurani.

2. Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba.
 
Ndio maisha yalivyo

wapo ambao pia walikimbiwa na Watoto wao wa kuzA na Mke wakaja kusaidiwa na Ndugu zao wakati wa changamoto na hali zilipotengamaa Mke na Watoto wakarejea wakaanza kusema Shangazi na Baba zetu wakubwa wabaya sana wanatugombanisha.

Hakuna maisha bila ya changamoto

swali ninalojiuliza

Dada yako alipata access vipi ya kuweza kuingia hadi chumbani na kuchukua nyaraka hizo muhimu na Mkeo hakujua kipindi chote hicho na House girl alikuwa anajua na hakusema hadi ulipomuuliza

Kama sio Movie nitabaki na mshangao sana

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom