Nishike mkono kwa kunipatia kazi yoyote halali

Hakuna kazi ya namna iyo usimuongopee mwenzio kila kazi ina taratibu zake.kwa maisha ya sasa uwezi pata kazi ya laki 6 bila kuonga
ulinzi nao mpaka uhonge? Mbona mimi nilipata bila kuhonga?

Ulinzi wa kuhonga labda pale bandarini (TPA) maana pale wanakunja pesa ndefu pamoja na marupu rupu inaweza fika hadi 900k.

Kwa hiyo unakuta hizo nafasi wale wajinga wanakuwaga wanaziuza (hongo)
 
Habari za asubuhi wakuu.

Ni siku nyingine tena, tumshukuru Mungu. Wakuu, nipo mbele yenu nikiomba msaada wa kibarua chochote ili angalau nipate 5000 kwa siku kwangu inatosha maana hali sio hali na nimepambana sana mpaka kufika huku kuomba msaada.

Kuna sehemu nilikuwa nafanya kibarua cha muda mfupi na nimemaliza muda wake week 2 zilizopita.

Wasifu wangu

1. Mwanaume
2. Umri miaka 32
3. Nina mke na watoto 2
4. Naishi Dar es salaam ila nipo tayari kufanya kazi popote
5. Elimu yangu diploma ya uhasibu ila sijawahi kuitumia kwenye harakati zangu
6. Nina leseni ya udereva class D


Naomba ndugu zangu kwa atakayeguswa na hili anipe support ili niweze kuilinda hii familia. Sichagui kazi

Asanteni. Asubuhi njema
Unaishi wapi, unapatikana wapi
 
Njooo PM nikupe kazi kama utakua haujapata ofisi ipo KIMARA jitahidi uwe unaishi sehemu ambayo usafiri kwako ni gari 1 tu kuja na 1 kurudi maana kwa 5000 unayotaka mimi nitakuongeza 2000 zaidi ya nauli jumla ntakupa 7000 tu.

Kwa elimu yako,sifa zako si haba tukapambana pamoja.

uwe tu mwaminifu na unionyeshe kwa vitendo maana halisi ya UAMINIFU.
 
Njooo PM nikupe kazi kama utakua haujapata ofisi ipo KIMARA jitahidi uwe unaishi sehemu ambayo usafiri kwako ni gari 1 tu kuja na 1 kurudi maana kwa 5000 unayotaka mimi nitakuongeza 2000 zaidi ya nauli jumla ntakupa 7000 tu.

Kwa elimu yako,sifa zako si haba tukapambana pamoja.

uwe tu mwaminifu na unionyeshe kwa vitrndo maana halisi ya UAMINIFU.
Mkuu asante sana nipo tayari kuja kuifanya hiyo kazi. Bado sijapata kazi. Mawasiliano haya 0766946609. Kuhusu UAMINIFU mkuu sitaki niongee sana ila utendaji wangu utajieleza
 
Back
Top Bottom