Nishati Safi: Kwanini Tunahimiza / Hamasisha kutumia Fedha za Kigeni katika Mapishi wakati tuna Mbadala

Logikos

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
14,919
23,539
Usinielewe vibaya mimi sio Mercantilist, na ninakubaliana na Bwana Smith aliposema, "It is the maxim of every prudent master of a family never to attempt to make at home what it will cost him more to make than to buy".

Kwahio cha kujiuliza je ?
Kuhamasisha matumizi ya LPG badala ya kuhakikisha watu wanatumia Umeme kupikia ni gharama ndogo au tunaweza kutengeneza LPG ?
Nadhani hapa jibu ni hapana LPG hatuna na inabidi tuagize kutoka nje na ni gharama kubwa zaidi hata kwa kipindi hiki ambacho vijijini unit inagharimu 100/=

Vilevile usinielewe vibaya mimi na Soko Huria ni Pete na Kidole na kama wafanyabiashara wa Gesi kina Oryx et al wanataka kuagiza gesi na kugawa bure au hata kuuza laki moja kwa mtungi huo ni uamuzi wao na wafanye hivyo, ila ni jukumu la Serikali na watumiaji wa Kodi zetu kutupa Alternative. That said inabidi tujiulize wale wanaogawa Mitungi ya Gesi vijijini (watunga sera / wawakilishi wa wananchi / watetezi wa wananchi) wanafanya hivyo kwa faida ya nani ? Sababu ukweli ni kwamba badala ya kusaidia wananchi wanatumbukiza kwenye matatizo zaidi


Je wale wanaosema Gesi ipewe Ruzuku ili Ishuke bei wanatutakia Mema ?
Ingekuwa hakuna mbadala ningewaelewa hawa watu, ila Ruzuku ni kwamba inatoka kwa mtu yuleyule ambae unampa ruzuku, yaani unachukua kwenye mfuko wake wa shati unamuwekea kwenye mfuko wake wa Kaptula (sababu hana hata pesa ya kununulia suruali); hivyo Ruzuku mwisho wa siku unamsaidia muuzaji na kwa case ya LPG mwisho wa siku ni mataifa ya nje, Sasa kwanini Ruzuku hii isiwekwe kwenye vyombo vya umeme ambao tuna uwezo wa kupata Nishati hii nchini ? Au kwanini siziende kwenye kuhakikisha umeme haukatiki na unakuwepo kila wakati na kwa bei ya chini Tanzania nzima ?

Hitimisho
Maswali ni mengi majibu sina.., hivi kwa kufanya tunachofanya (Kupigia chepuo Nishati ya Gharama kubwa, wakati tuna Alternative) ni kwa faida ya Nani ? Sikatai wauza gesi wenyewe wafanye huo Udalali lakini sio Serikali / Wawakilishi wetu ambao kazi yao ni Kututetea ila kinachoendelea sasa hivi wanatuangamiza.

For once tuwe wazalendo na tumsaidie Mwananchi..., Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichonacho, Tufanya Tunachoweza.


 
Back
Top Bottom