BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,820
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za Mafuta ya Petroli zitakazotumika kuanzia Desemba 6, 2023 ambapo Dar es Salaam Petroli ni Tsh. 3,158, Tanga Tsh. 3,204 na Mtwara Tsh. 3,231 kwa Lita moja ya Mafuta.
Dizeli Dar es Salaam itauzwa kwa Tsh. 3,226, Tanga Tsh. 3,377 na Mtwara Tsh. 3,546. Mafuta ya Taa yamesalia kwenye bei za Novemba ambazo ni Tsh. Dar es Salaam 3,423, Tanga Tsh. 3469 na Mtwara Ths. 3,495 kwa Lita moja ya Mafuta.
EWURA imesema Bei za Mafuta (FOB) kwa mwezi Desemba zimepungua kwa wastani wa 0.86% kwa Petroli na 9.11% kwa Dizeli. Pia, gharama za uagizaji Mafuta kwa Bandari ya Dar zimepungua kwa 24% kwa Petroli, 30% kwa Dizeli. Tanga gharama za kuagiza Petroli zimeshuka kwa 30% na 17% kwa Dizeli.
==========