Duniani kote nchi zilizoendelea zinategemea uwepo wa nishati bora katika kufanya shughuli zake, nchi maka Marekani, Urusi, china na nyinginezo zimeendelea kwa sababu ya ubora wa nishati wanayoitumia.
katika miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania kumekuwa na jitihada mbalimbali za kusaidia kuleta mabadiliko hasa katika nishati ya umeme lakini hatua hizo mwaka hadi mwaka zimekuwa zikionekana kutozaa matunda mazuri kwa suluhisho lake hudumu kwa mda mfupi tu na tatizo hilo kuendelea jambo ambalo limekuwa likitatiza sana shughuli mbalimbali hasa za kiuchumi kama vile viwandani kwa kukosa nishati bora.
kwa utafiti wangu mdogo niloufanya katika miaka kadhaa nimekuja kugudua kuwa kuna sababu mbalimbali zilizochangia tatizo hili kama vile nishati si toshelevu ukilinganisha na matumizi ya watu, ubovu wa mitambo ya kuchakata umeme, usimamizi mbovu wa sekita husika na uhujumu unaofanywa na wanachi kwa kuiba na kuharibu baadhi ya miundombinu.
Hivyo upo umuhimu kama nchi wa kufanya maboresho kadhaa ili kuweza kuleta mabadiliko mbalimbali kwani bila kuwepo kwa mikakati thabiti suala la ubora wa nishati litakiuwa ni gumu kupatikana katika nchi yetu, mambo ya kufanya ni kama yafuatayo;
shirika la umeme lisisimamiwe na serikali, katika vipindi vyote tumeona nguvu ya serkali katika mashirika yanayojihusisha na nishati jambo ambalo limekuwa likisababisha baadhi ya viongozi kutoa kauli za kisiasa katika mambo ambayo yanahitaji utaalamu, jambo hili limekuwa likirudisha nyuma sana maendeleo ya nishati ya umeme kwani kauli za kisiasa zimekuwa zikitumika kuwaaminisha watu juu uwepo wa nishati hii ilhali si jambo la kweli
Pia serikali itangaze tenda kwa mashirika binafsi lililotayari kushika tenda ya kuzalisha nishati ya umeme. mashirika hayo baada ya kutangaziwa yapeleke dodoso lao na namna yatakavoleta mabadiliko katika nishati hii ya umeme, baada ya hapo waliowasilisha ombi wasindanishwe ili kuweza kupata mshindi na akipatikana ndiye apewe kuzalisha nishati ya umeme, akifeli kwa mda atakaopewa utakaokuwa ni mda wa matazamio atakuwa amejivua moja kwa katika tenda hii.
kitu kingine ambacho serikali ifanye ni kuiondoa nishati ya umeme kutoka gridi ya taifa na kuigawa katika mikoa, hapa namaanisha kila mkoa utafute chanzo kizuli cha maji na ufue umeme wa kwake na utumike katika mkoa huo pekee, unapogawa kitu na kwenda katika ngazi ndogo usimamizi unaweza kuwa mzuri zaidi, watu wasitegemee umeme kutoka gridi ya taifa baadala yake kila mkoa uwajibike kupata nishati yake.
Pia, jambo lingine ni kuhusiana na nishati mbadala, nchini Tanzania tumejikita zaidi katika umeme wa maji, hatuna uoni wa kutazama vyanzo vingine kama kutengeneza vinu vya nyukilia vitakavyozalisha umeme, nchi mbalimbali zinapambana katika kuwa na mbadala wa nishati mbalimbali, hivyo na Tanzania ufanyike utafiti wa vyanzo hivyo mbadala.
Mwisho, maendeleo ya nchi yetu yanategemea sana uwepo wa nishati bora, kama Tanzania itaamua kufanya mabadiliko katika suala la nishati ya umeme maendeleo yatakuja kwa kasi na tunaweza kuingia katika orodha za nchi bora zilizoendelea katika masuala mbalimbali kwa nishati ya umeme ndiyo inayozibeba nishati nyingine zote.
Nishati safi kwa usitawi wa vizazi vijavyo.