Nisaidieni vitu gani vya kukagua inaponunuliwa injini used?

salari

JF-Expert Member
Jan 22, 2013
2,775
4,857
Habari wanajamii forums!

Naomba mnisaidie ni vitu gani vya kukagua mtu anaponunua njini ya gari ambayo ni mtumba/used. Vilevile ni vitu gani vya kuzingatia. Nahitaji msaada huu maana nitanunua hiyo kitu hivi karibuni. Nimejaribu kuulizia uzoefu kwa watu ambao washanunua baadhi yao wanalalamika kwamba injini walizonunua majanga matupu! Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wote watakaonisaidia.
 
Kama una mtu unamfahamu tunduma mwambie akufanyie mpango... zinatolewa Kwenye IT zilizotelekezwa kwenye makazi ya watu .
 
Salari,

Siku hizi watu wamekuwa wajanja mno. Engine nyingi zinazouzwa zinakuwa tayari zimefanyiwa overhaul au nyingi zinakuwa zimeshapata ajali hapa nchini.

Unaweza kuwasha engine ya diesel kabla ya kununua, lakini haitakupa picha kamili kama ni nzima. Na hata kama ukichukua fundi, mafundi wengi ni watazamaji tu na wengine huwa wanakupeleka kununua na wanapewa percent zao.

Kikubwa ni kununua kutoka trusted companies au maduka, wanaogazia nje ya nchi wao kama wao. Zungukia makampuni yanayoagiza.
 
Kiongozi,

Engine uliyonayo imekufa kabisa? Hivi hapa TZ hakuna watu/kampuni au gereji inayoweza kufanya OVERHAUL ya engine kwa kuzingatia taratibu zote na injini ikarudia upya?

Pengine tatizo ni vipuri, wafanyabiashara wakubwa waanze kuwekeza kwenye kuagiza vipuri vya magari, mafundi wa ku-overhaul injini naamini wapo wengi tuu.

Nitapendelea zaidi injini iliyofanyiwa overhaul ya uhakika kuliko injini ya mtumba.
 
Injini hasa ni cylinder head cylinder block vingine ni vikorokocho vya kujazia tu, unaweza kununua madukani tatizo ni gharama kununua kifaa kimoja kimoja ndo maana watu wanaamua kuagiza mitumba ya injini kutokea nje ya nchi.
 
Injini huwezi kuikagua kwa kuiangalia tu. Injini kwa kadili inavyofanya kazi crank shaft inasagika na kuwa kama muundo wa pai, hii inafanya mzunguko wa injini kuwa sio mzuri kwani injini inakuwa nzito(haina kasi), pia kuna pistons, cylinder block(injini nyingi zilizokufa huwa zinaenda kuchongwa block ambazo piston hukaa ndanibyake). Kwenye cylinder head unaweza ukakagua valves + springs, lakini mimi nadhani kuikagua injini ni lazima uiweke kwenye gari na uendeshe uone kama ni nyepesi au nzito, kumbuka injini zinazoingizwa bongo ni mitumba, kwahiyo usitarajie kula bila kuliwa.
 

Mkuu "Sir With Love" nisaidie trusted companies au maduka hayo kama unayajua!
 
Lahaula lakwata ukweli mchungu huu! but shukrani sana kwa kunijuza!
 

Mkuu Ndalilo injini haijakufa, gari inatembea ila ina mlio balaa yaani ningepata hao wataalamu wa kuoverhaul ingekuwa poa pia!
 
Lahaula lakwata ukweli mchungu huu! but shukrani sana kwa kunijuza!
Nenda kariakoo pale kuna duka kubwa sana nimesahau mtaa lilipo, linaitwa kisangani, nilisikia umaweza weka order ya injini au spea yoyote wao wakakuletea.
 
Kwanza tafuta fundi mzuri halafu njia rahisi ni kufungua sample ya chini na ukague size ya crankshaft/Main/Cones. zikiwa bado ni standard basi hiyo engine ni nzuri.
 
Kwanza tafuta fundi mzuri halafu njia rahisi ni kufungua sample ya chini na ukague size ya crankshaft/Main/Cones. zikiwa bado ni standard basi hiyo engine ni nzuri.
Yap yap Abunuwasi thanks sana mkuu dah kumbe kuna kufungua sample hapa!
 
Nenda kariakoo pale kuna duka kubwa sana nimesahau mtaa lilipo, linaitwa kisangani, nilisikia umaweza weka order ya injini au spea yoyote wao wakakuletea.
Ok! Ok! mi nlijuaga Kisangani wanauza spare parts mpya tu kumbe wanauzaga na used pia thanks kwa info!
 
toyota belta, cc1497 VVTi, valve 16. si ndio mkuu.. iyo mkuu engine inahitaji overhaul kubwa tu stage ya engine kufikia kupiga kelele km usemavyo kuna vitu vinashida mkuu hasa kwe cylinder block, crank shaft kupiti con rod,had kwe piston hali si shwar..xo iyo ela ya kununua engine mkuu bora uende toyota kwanza kawakabidhi iyo gari ikitoka huko utafurah mwenyewe..cz wale jmaa ndo watakuambia wenyewe kuwa hii haifai tena or vp..so fanya ivo nenda Toyota mkuu.
 
toyota wapi?, china au
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…